Katavi
SERIKALI imesema kuwa haina mpango wa kuwakopesha fedha wachimbaji wadogo bali imeahidi kutatoa mikopo wa vifaa baada ya kubaini kuwa fedha zilizokuwa zikitolewa awali wachimbaji hao zilikuwa hazitumiki kama ilivyokusudiwa.
Naibi Waziri wa madini Doto Biteko aliyasema hayo jana wakati alipokuwa akiwahutubia wachimbaji wadogo wa madini wa mkoa wa Katavi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika machimbo ya dhahabu ya Ibindi Wilayani Mpanda.
Alisema kuwa
Wizara ya madini imeamua kuondoa
utaratibu wa hapo
awali wa kuwakopesha fedha wachimbaji wadogo kwa ajiri ya kununulia vifaa
vya kufanyia shughuli za uchimbaji na badala yake watakuwa
wanawakopesha vifaa.
Waziri huyo alisema kuwa fedha
zilizokuwa zikitolewa na
Serikali kwa ajiri ya kuwakopesha wachimbaji
wadogo zimekuwa hazitumiki
kama ilivyokusudiwa na
badala yake wamekuwa wakizitumia kwa matumizi
mengine.
Alieleza
wachimbaji wadogo wamekuwa
wakikopeshwa fedha kati ya shilingi Milioni 100 na milioni 200
lakini badala ya
kununua vifaa vya
kuchimbia madini wao wamekuwa wakizitumia kwa ajiri ya kununua
magari na kujengea nyumba .
Alisema kuwa wachimbaji
wadogo wote walikopeshwa
fedha na wakashindwa
kuzirudisha wanatakiwa wazirudishe
mara moja kwani kwa
wale watakao shindwa kurejesha
watakamatwa na kufikishwa
mahakamani .
Aliwataka wachimbaji
wote wa madini hapa
nchini wawe waaminifu
kwenye kulipa kodi
za Serikali na wachimbaji
wadogo waache tabia yao ya vichochoro
vya kusafirisha madini kwa
njia ya magendo kwani mchango wa
sekta ya madini bado ni
mdogo kwenye mapato ya
Taifa kutoka na
madini mengi kuzushwa nje ya
nchi .
Alisema Serikali
haiko tayari kuona
kazi zinazoweza kufanywa
na Wanzania kwenye
migodi ya madini
zinafanywa na watu wa kutoka
nchi za nje kwani lengo la Serikali ni kutaka kuona Watanzania
wananufaika na rasilimali za
madini .
Mwenyekiti wa Chama
cha Wachimbaji wadogo wa Mkoa wa
Katavi Willy Mbogo
aliiomba Wizara ya madini
kutunga sheria ambazo
zitakuwa zinawapa nafuu
kwani sheria za
sasa haziangalia aina ya
wachimbaji wadogo na wakubwa .
Alisema
yapo maeneo ambayo
ambayo baadhi ya wachimbaji
wanayamiliki kwa kuwa na
leseni lakini yamekuwa
hayaendelezwi hivyo ni
vema serikali ikawafutia
leseni wachimbaji hao .
Katibu wa
chama wa wachimbaji
wadogo wa Mkoa huu
Filberti Sanga aliomba
wizara ya madini
iwafutie leseni wachimbaji
ambao wachindwa kuyaendeleza
na bbadala yake wapewe wachimbaji wadogo .
Alisema
wapo wamiliki wa leseni
za madini ambao
maeneo yao hawayaendelezi
wamekuwa wakibadili majina
kila muda wao
wa leseni kumalizika
kwa kuhofia kufutiwa leseni zao .
Mwisho