Friday 29 May 2015

Siku ya pili ya kongamano la FIFA imeaanza

Blatter anakabiliana na mpinzani wake mkuu mwanamfalme Hussein kutoka Jordan
Siku ya pili ya Kongamano la kila mwaka la FIFA imeanza huko Zurich Uswisi.
Siku ya pili ya Kongamano hilo ndio inayomchagua Rais wa FIFA.
Awali kumekuwa shinikizo kwa FIFA kuhairisha kongamano hili na pia uchaguzi wa urais.
hata hivyo maombi hayo yalifutiliwa mbali na inatarajiwa kuwa rais Sepp Blatter ataendelea mbele na uchaguzi ambao anakabiliana na mpinzani wake mkuu mwanamfalme Ali Bin al Hussein wa Jordan.
Blatter alifungua kongamano hilo kwa kuomba kuweko na umoja miongoni mwa maafisa wa FIFA.
Amesema kuwa tuhuma hizo ni njama ya kuibua maswali dhidi ya uwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa 2018 na 2022.

Blatter amesema kuwa tuhuma zinazoenea sasa ni njama dhidi ya FIFA
Blatter aliyasema hayo alipokuwa akiwahutubia wajumbe, katika siku ya pili ya mkutano mkuu wa shirikisho hilo la kandanda duniani huko Zurich Uswisi.
Blatter ameahidi kukamilisha mabadiliko yatakayoirejeshea FIFA hadhi yake.
Blatter anakabiliana na mwanamfalme Ali Bin al Hussein wa Jordan katika uchaguzi huo utakaofanyika leo.
Kwa upande wake mwanamfalme Ali Bin al Hussein wa Jordan anasema kuwa yeye pekee yake ndiye aliye na nia ya kuleta mabadiliko ya kimsingi yatakayomaliza ufisadi na ulaji rushwa ndani ya FIFA.
Takriban wenyeviti wa mashirika 209 ya kandanda kote duniani wanakura moja kila mmoja .
Mwaandishi wa habari wa BBC, anasema kuwa Bwana Blatter anategemea uungwajji mkubwa kutoka kwa wajumbe wa mataifa ya Amerika, Afrika na Asia - ambao wanasema kuwa amefanya mengi katika kuboresha mchezo wa kandanda katika mataifa maskini.
 
FBI inachunguza uwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa 2010
Naye Prince Ali anauungwaji mkubwa kutoka mataifa ya bara Ulaya.
Wajumbe hao wawili watahitaji zaidi ya robo tatu ya kura zote ili kupata ushindi wa moja kwa moja katika mkondo wa kwanza.
Hilo lisipofanyika, kutakuwa na mkondo wa pili wa upigaji kura, ambapo mshindi wa kura nyingi atatangazwa mshindi.
FIFA imekabiliwa wimbi la tuhuma za ufisadi ulaji rushwa na ubadhirifu mkubwa baada ya maafisa wake wakuu saba kukamatwa na polisi nchini Uswisi ilikujibu mashtaka nchini Marekani.
Maafisa wa kijasusi kutoka Marekani FBI wamependekeza kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa maafisa 14 wa FIFA kwa kula mlungula wa takriban dola shilingi 150 katika kipindi cha miaka 20.

Vijana 85 wenye itikadi kali wajisalimisha Kenya

Serikali ilitoa msamaha kwa wale wote waliojiunga na Al Shabab baada ya kuuawa kwa wanafunzi 150 mjini Garissa
Takriban vijana 85 waliokuwa wamepokea mafunzo yenye itikadi kali wamejisalimisha kwa polisi nchini Kenya.
Vijana hao wamejisalimisha kwa serikali ya Kenya, ili kupokea msamaha uliotelewa kwa wale wote ambao wamepokea mafunzo ya itikadi kali ya kiislamu na kujiunga na kundi la wapiganaji wa Al-Shaabab.
Msemaji wa Serikali imesifu hatua ya vijana hao, akitaja kuwa itachangia pakubwa ukusanyaji wa taarifa za kijasusi.
 
Vijana 85 waliopokea mafunzo yenye itikadi kali wajisalimisha kwa serikali ya Kenya
Awali vijana hao walihofia kujisalimisha kwa hofu kuwa wangetengwa katika jamii na hata kufungwa gerezani.
Maafisa katika wizara ya mambo ya ndani wamesema kuwa vijana hao walikuwa kati ya umri wa mika ishirini na thelathini.
Serikali ya Kenya iliahidi kuwasamehe vijana hao mapema mwezi uliopita, kufuatia uvamizi katika chuo kikuu cha Garissa, ambapo zaidi ya watu 150 waliuawa.
Kundi la wapiganaji wa Kiislamu wa Al Shabaab walikiri kutekeleza shambulizi hilo ambalo limepelekea chuo hicgo kufungwa.

Al Shabaab inaitaka Majeshi ya Kenya yaondolewe Somalia
Kujasalimisha kwa vijana hao kumepiga jeki juhudi za serikali ya Kenya dhidi ya mafunzo ya itikadi kali, yanayochangia hatua ya vijana hao kujiunga na makundi ya kivita kama vile Al Shabab.
Kundi hilo kutoka Somalia linaaminika kuwa na wafuasi nchini Kenya ambapo limetekeleza mashambulizi kadha katika jitihada ya kuilazimisha serikali ya Kenya kuondoa majeshi yake nchini Somalia.
Majeshi ya Kenya ni miongoni mwa kikosi cha kulinda amani cha muungano wa Afrika Amisom ambao wanaisaidia serikali dhaifu ya Somalia kupigana na waasi wa Al Shabaab.

Diamond Platnumz''Kukutupa'' jiwe jipya kesho


Nyota wa muziki wa Bongo flabva nchini Tanzania, Diamond Platnumz anatarajia kuachia ngoma mpya ya kimataifa ambayo mpaka sasa haijajulikana kwani tayari ameshafanya collabo na wasanii watatu wa kimataifa akiwepo Flavour, P-Square na nyota wa Kimarekani.
 
Diamond ameshare picha ya fomu yakeya kutuma videoya wimbo wake ‘Nana’ ambayo ni collabo yake na Mr Flavour kwenda BET International, video iliyoongozwa na Godfather wa Afrika Kusini inayotarajiwa kutoka May 29, 2015.
 
Aidha meneja wa Diamond, Babu Tale amesema kuwa watanzania na mashabiki wa muziki wa Diamond wasubiri Ijumaaa ifike watajua kuwa ni collabo gani wataachia kwani tayari wamefanya collabo nyingi za kimataifa.
 

Issue ya Shilole yatua mjengoni


Sakata la Mwanamuziki Shilole kucheza  huku baadhi ya sehemu za matiti zikiwa wazi limechukua sura mpya Bungeni leo kufuatia Naibu Waziri wa Habari vijana na Utamaduni na Michezo Juma Nkamia kutangaza kuwa  inasubiria uamuzi wa Baraza la sanaa Taifa (Basata).
 
Aidha, Nkamia amesema   suala la shilole hivisasa lipo chini ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)  ambapo mara baada ya kumaliza mahojiano naye litapelekwa wizara ya habari vijana na utamaduni  na michezo kwa hatua nyingine zaidi.
 
Hivi karibuni Shilole  aliwaomba  msamaha watanzania  kwa madai kuwa anajutia kutozingatia maadili katika onesho hilo lililofanyika nchini Ubelgiji na  kuzua gumzo nchini Tanzania.

PPRA YAWAPIGA MSASA WAFANYAKAZI WA TIA KUHUSU SHERIA MPYA YA MANUNUZI JIJINI DAR

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjrO5bfErWirGj5FKJ7NNI8qE4j0VZ76REXh2Ty1CaBeXT1FOeCe17efoOBndHEGwPe3vDHEHNzzkWim9EB7P2j4qibrWxfs4DPE2WdLWlc1WNORHAVdo9jNyez5ZhOk8xKiSBfQcEq1M0/s1600/IMG_6868.JPG



Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania(TIA) Dkt.Joseph .M.Kihanda mwenye suti nyeusi(waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Mafunzo maalum kuhusu sheria mpya ya manunuzi ya umma yaani PPA 2011 na kanuni zake PPR.2013 ambao ni wadau wa kitengo cha manunuzi kinachosimamiwa na Bi.Juliana Musomi,Pius Seda,Salha Tego,Dickson Biya,Ezra Obilla,Kennedy Ndosi,Zubeda Mohamed,Alton Kumburu  na Stephen Mahinya),wajumbe wa bodi ya zabuni ya Taasisi hiyo ambao ni Bw.Zodo .M.Zodo,Bi.Linah Tumwidike,Bajjet Naresho,Anthony Mzurikwao,Said Mayunga,Lucina Comino na Burkad Haule pamoja  na wawezeshaji toka Mamlaka ya udhibiti wa ununuzi wa umma (PPRA) ambao ni Bw.Gilbert Kamnde akishirikiana na ,Onesmo France,pia washiriki wengine walikuwa ni mkurugenzi wa biashara wa Taasisi hiyo Bw.Mzee Boma na  mameneja wote wa matawi ya Taasisi hiyo ambao ni  Ndugu John Boneka(Kigoma)Bw.Emmanuel Kingu (Singida),Luciana Hembe Mwanza)Bw.Mugisha Kamala (Mbeya na Bw.Matei Mapunda(Mtwara).

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgHNp-5hOShN62KzjZv-j2S05aHe4V1klXdxi5i2-A0MxTaC83ASpQrIAVYjkj8McnzhehH6lYZJdYFerAoioJYUnkqGeSXjJOuDS_rcZZArljaDVOffYnjS_Cuvrq1yh0PF1BXK3oy2G8/s1600/IMG_4302.JPG



Wasiriki wakiwasikiliza wawezeshaji kabla ya kumalizika kwa mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa baraza la maaskofu wa kanisa katoliki Tanzania T.E.C Kurasini jijini Dar es Salaama kwa siku tano kuanzia tarehe 25/5/2015 hadi tarehe 29/5/2015 ambapo washiriki watatunukiwa vyeti vya mahudhurio toka PPRA.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi6wgcxAY9J7dS5AMOMjeqA1T19Fhf3bQIgHQASMCxB1aBnd3UT9ADXUkcLsas3sJQETPr2i6JLnazAbpflYa5qsV8pVJFY08PNQq7Snj2RiXpvZ7rxvEsQfenTciGhfIHSxd70uj9bntw/s1600/IMG_4294.JPG



Mkuu wa kitengo cha Manunuzi wa Taasisi hiyo akiwa anaendelea kufuatilia kwa makini mafunzo hayo ambapo amekiri yatasiadia kuongeza ufanisi katika kitengo chake na Taasisi kwa ujumla hivyo kuomba Afisa mtendaji mkuu kuwawezesha mafunzo mbalimbali yanayohusu manunuzi ili Taasisi iendelee kufanya manunuzi kwa kuzingatia thamani ya pesa yaani '' Value for Money Procurement'' na kuiletea Taasisi Sifa nje na ndani ya Nchi kwani inatoa pia mafunzo katika ngazi ya cheti hadi Postgraduate kwa masomo hyo ya ugavi,ughasibu na mengine mengi katika nynja ya biashara.

MKUU WA MKOA WA DODOMA MHE. CHIKU GALLAWA AMUAPISHA MKUU MPYA WA WILAYA YA MPWAPWA MHE. ANTH0NY MAVUNDE

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgVRPzTqCr6rFAnC8s1Wx3G1Qyv0HwSTi_h-4tSqcFKsY6sWB41_GLqZb3UuEVHrkLQVBtyH_u970bd6cPikkFPb0GhMTKbEBy9VvJiyCDqum5TWfXXXcypXR6qWvTAGsVsEttEJiG-wqvW/s1600/1.JPG


Mhe. Athony Mavunde akila kiapo cha kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (Hayupo Pichani) Mei 29,2015

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgyC3IVmJMkNzy-cZlx0cPu9ZK6oasbjutjh7S0Td-kD8iDbgJeaFAhGW-FxI8WVNEx-W1YRTBMREI6oJhjJeykbybs7DkQATukiY9Y8HzKygmecahkhzovoTGgvgACvkqZGSKISmi7qOTb/s1600/2.JPG

Mhe. Athony Mavunde akitia saini hati ya kiapo cha kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa Mei 29,2015

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiKhk1puT4CfRyRVcvnSsVHK9zJ_3-ZeYeKqzMdSuZWcZCYDAl9L_YtY3BXhRvs8ZXnaM0RDx-Gpa5XEIpoiIIG4Wc4-66Jd8wktV2VpkEFtTXCyxLuluMn69uyHFPru4TIX-Z8wkghH-Ke/s1600/3.JPG

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Athony Mavunde (kushoto) akipongezwa na baba yake mzazi Ndg. Peter Mavunde mara baada ya kula kiapo cha kuwa Mkuu wa Wilaya Mei 29,2015
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjGcMza6MaposnLIkUWWO0zTtYI9sdB3UrEROqbike8LNC4lVmTmerhqQn3a-rduybhyphenhyphengY039FkoWJFFxaPVz9Zvg7riVqsrms8OrmHXq1uDhM-sTxEjPixt6JQYr_tgqZQMSspADkfSf08/s1600/4.JPG


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Athony Mavunde (kushoto kwake) na wajumbe wa kamatiya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Dodoma wakati wa Hafla ya kumuapisha Mkuu huyo mpya wa Wiaya ya Mpwapwa Mei 29,2015

WAZIRI MKUU PINDA AHUTUBIA SHEREHE ZA MIAKA 25 WA TAWLA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEioMLOSYeQgoRODWi5BMjj_LfAuhxMv6mTsS7r1_NA_FQOhc0Wi7yIj3N7-8mj9stzgeRO8sOtbKxjvgHz6_uBwHMFEh3NJO_P_r8S0SlZhn15wE2crWdD_cHXepk3IZqA0tIRBX8l842_t/s1600/IMGL7391.JPG


  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza wakati alipozindua Uandishi wa
Wosia katiak sherehe za miaka 25 ya Chama cha Wanasheria Wananwake
(TAWLA0 kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam Mei 30,
2015.Kushoto ni balozi wa Sweden nchini, Lennarth Hjelaker


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjS5XpRshgGkp58excMHPNKvQYbT_7iaAyCzPdjqGRIllxz6_2gykUyPrrv2yyLMLisUrftVP0izA0wynQyrwRMm8AGiUdmV4sMfJUZyQhgiXPpA1y50_-da5cqAVTAFonryuTasWrv9P9B/s1600/IMGL7452.JPG

 7452  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na
Balozi Mwanaidi Maajar baada ya kuhutubia katika sherehe za siku ya
Wanasheria Wananwakde Tanzania Tawla , kwenye viwanja vya  Karimjee
jijini Dar es salaam Mei 30, 2015.



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhsL28YPlL-H6Wo2In6XwoWVq2ojJ_p2ME4XUaevLUwnhW-07X-wxlfbznrTKK0Xh-9ws7oCaeiUcam5wl8Hkc5noLnFE_PqPT4QqLz2doigWLuLd63dAvnArKQnz0rj-8ZGA8SbITGSyKT/s1600/IMGL7506.JPG
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Balozi wa Sweden Nchini, Lennarth
Hjelaker baada ya kuhutubia katika sherehe za kuadhimisha miaka 25 ya
Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) kwenye viwanja vya
 Karimjee  jijini Dar es salaam Mei 30, 2015.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEihDuSUawkqTG9Cd0EoQZGQ0gpE1gk6_Lt4cwoLo4Wp5Zzlc-WLXhDxfmuN1qX7Ov2j5oEYq_on3k7SWh1VlkULk3eoKU5cvHP3xma2mOEvjcUSC4b3psbSfkH3gtbAAn9dLJ_cWYcf_jiZ/s1600/IMGL7426.JPG

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
wanachama wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) baada ya
kuhutubia katika sherehe za miaka 25 ya chama hicho kwenye viwanja vya
 Karimjee jijini Dar es salaam Mei 30, 2015. Aliyekaa wapili kulia ni
balozi wa Sweden nchini, Lennarth Hjelaker.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiTGdHHEPf8xXiTuZXXXEoBrj4oJtc39DrkZ0tEYzVvhxVW0CsX3n2-1hULQCdZ-OYIbPy9jh1io7bt7lVqRgwvwyWyM2y0N6l8QpW79E2oZwvXjzR2T7QJwkEKjqVDjDGWbWRkgL9r2WsA/s1600/IMGL7337.JPG

   Baadhi ya wananchama wa Chama cha Wanasheria Wananwake (TAWLA)
wakipita kwa maandamano mbele ya mgeni rasmi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
katika sherehe za miaka 25 ya TAWLA zilizofanyika kwenye viwanja vya
Karimjee jijini Dar es slaam Mei 30, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu).

Serikali yatangaza kutenga bajeti zaidi kwenye tafiti za afya.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhOWUqGpUVjZ88cJrCVLA0l2mWtqPHkvmwbTcDQ4VwO8FNjDKJx7y2YOpCFstahc2glSZhITF2XC_H-p6A_rtq3d-P4sHApLMQfFuaAqQkrG76Prix51EWpfL1pCz9tVoVMPfJFUDFvOg4/s1600/PICHA+1.JPG


 Naibu wa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi, Mh. Anne Kilango  akisisitiza jambo  mbele ya  Madaktari na wanafunzi wa udaktari kutoka Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) waliohudhuria Mkutano Mkuu wa tatu wa sayansi ya afya ulioandaliwa na chuo hicho  jijini Dar es Salaam jana. Kwenye mkutano huo wa siku mbili huku ukilenga  kujadili masuala ya tafiti kwenye sayansi ya afya, Mh. Kilango alimuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Mohamed Gharib Billal.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjH_Cis3J-xeNdQ0PXGezPcN83EvJs-uPLvsmt1-bv8wWGep3cveQb5vdh7oCY5wezeRP8aQ9rB9h6rG_LRXd2P449pLZigpgiS8LEHpqAn28lyPuQk0Bhm_xu_4R-l8Lc0NY1u6JE5EZ4/s1600/PICHA+2.JPG

 Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Anna Kilango (kulia) akijadiliana jambo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof.Ephata Kaaya, mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa tatu wa sayansi ya afya ulioandaliwa na chuo hicho  jijini Dar es Salaam jana.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi4VKghpmJuFgPFpN7Nb8zqIVKlxsakS6hJN5OOaVUFQGBysfj4ZTFOqIAV80XpgbJSyFC5pj8KrfHhN_4sc0cxFiyGSJppyyDE7e44YxsCY0msqlY9zJ1Bfve7fFeaBnN0lflAOgPELj0/s1600/PICHA+3.JPG
Baadhi ya wanasayansi, Madaktari na wanafunzi wa udaktari kutoka  Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) wakifuatilia kwa umakini Mkutano Mkuu wa tatu wa sayansi ya afya ulioandaliwa na chuo hicho  jijini Dar es Salaam jana.

Naibu wa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi, Mh. Anne Kilango  amebainisha kuwa bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2015/16 imeongeza fungu zaidi kwenye masuala ya utafiti hususani ule wa sayansi ya afya.

Mh. Kilango alitoa kauli jijini Dar es Salaam jana wakati akifungua  Mkutano Mkuu wa tatu wa sayansi ya afya ulioandaliwa na Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) na kuhudhuliwa na mamia ya Madaktari na wanafunzi wa udaktari kutoka chuo hicho.

“ Ili taifa liweze kufanya vizuri kwenye sekta yoyote ile ni lazima tuwekeze zaidi kwenye masuala ya tafiti. Kwa kulitambua hilo napenda kuwataarifu kuwa hata kwenye bajeti yetu ya mwaka huu wa fedha tunatenga kiasi kikubwa cha rasilimali fedha kwa ajili ya kuwezesha tafiti hizi zikiwemo hizi za masuala ya afya,’’ alisema Mh. Kilango ambaye alimuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Mohamed Gharib Billal.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof.Ephata Kaaya alisema kuwa kwa sasa taifa linahitaji zaidi tafiti za kiafya hususani kwenye magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo kisukari, shinikizo la damu na saratani.

“ Ni dhahiri kuwa kwa sasa magonjwa haya yasiyo ya kuambukiza yamekuwa ni tishio kwa taifa. Kama wataalamu wa masuala ya afya tunaona kuja tija zaidi tukiwekeza katika tafiti zinazohusu pia magonjwa haya,’’ alibainisha.

Mkutano huo wa siku mbili unatarajiwa kuhitimishwa leo ambapo zaidi ya tafiti 100 kuhusu maswala ya afya zitawasilishwa.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUDHURIA KUAPISHWA RAIS WA NIGERIA LEO

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhfOJ_-q0krUtEd1SoCOCoz8UHkyYRllJUqy9BKS6fiWnkubBSqq166_BC-6ksS6P7HbIP4_7nyrdQKW5F5rKnao0emVKKFy1bOwOh3zBx41NPoNUKGR_9AUfXwgnbyhInr-utV4jhAY-c/s1600/IMG_8504.JPG


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na mtoto Ernest Nkayala alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria. 

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjvEdufb0opWBtj8vHaWNYwxsDyJlK8q8d0pemtF73F8Yok0abzXtowFx1MmuSHwJ9M8q1cE3lV_IxSW9TZGLznhP_SkI62ZZ-Ivsw1dajXh5JhNoYAAl5LsNqd1dvUcGSXDClwRBMTNzw/s1600/IMG_8508.JPG

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mkewe Mama Asha Bilal, wakiwasili kwenye Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiyN9HmWbL6xUiZOL7iFvNFVBsacRxR-PFIx13KAo9f9_CjBGFbspgQg1uCPQ-WfCGCLmKUlaQrWTrpsgT66L6wkhCGhc6PDxmZrlCttb_sZ8dWGjx-X6-jJvY3XclFA6f69A2GAqebrDk/s1600/IMG_8518.JPG

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea shada la maua kutoka kwa Mtoto Elin Mwandobo alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.




https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj7bBN90gouUCYP1Hoh_Kj_qWBEG2zlHPFG-wVFSxaNH7CpGk3_ZXD5pEGhYyKDBVCSoNkAlKs9PzbzhUeudJEfeDS9RK_5FYDmMsoRA8UJ0_ATzoUxiea1guyrwFz4HvwG_dmc1et3SbU/s1600/IMG_8525.JPG
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia ngoma za kabila la Kinigeria alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.

(Picha na OMR).

Mlipuaji wa kujitoa mhanga awaua 4 Saudia

Mlipuaji wa kujitoa mhanga awaua 4 Saudia
Watu wanne wameuwawa baada mlipuaji wa kujitolea mhanga kujilipua nje ya msikiti mmoja wa waislamu washia nchini Saudi Arabia.
Duru zinasema kuwa watu kadhaa wamejeruhiwa, katika mkasa huo uliotokea katika mji wa Dammam, katika jimbo liliko Mashariki mwa taifa hilo.
Dammam ni makao makuu ya jimbo la mashariki, kuliko na waislamu wachache wa Washia.
Juma moja lililopita, watu 21 waliuwawa baada ya mlipuaji wa kujitolea kufa, alipojilipua ndani ya msikiti mmoja wa katika kijiji kimoja jimboni humo.

Uhasama wa kidini umekuwa ukitokota baina ya madhehebu ya Sunni na Shia kufuatia mashambulizi ya Saudia nchini Yemen
Uhasama wa kidini umekuwa ukitokota baina ya madhehebu ya Sunni na Shia kufuatia mashambulizi ya Saudia dhidi ya Washia.
Taharuki inazidi kuikumba Saudia, hasa baada ya ndege za Saudi Arabia zilipoanza kutekeleza mashambulizi ya angani dhidi ya waasi wa kishia wa Huthi, katika nchi jirani ya Yemen.

WAKATOLIKI WAJIONDOA KWENYE UCHAGUZI BURUNDI


Kanisa Katoliki nchini Burundi limejiondoa katika mchakato mzima wa uchunguzi na uongozi wa aina yoyote katika uchaguzi huo.

Uamuzi huo umekuja wakati ikisalia wiki moja tu uchaguzi wa wabunge na madiwani ufanyike nchini humo
Kanisa katoliki ni kiungo muhimu katika suala la amani na demokrasia nchini Burundi tokea kuanzishwa mazungumzo ya amani ya Arusha mnamo miaka ya tisini.
Haya yamearifiwa wakati maandamano dhidi muhula wa tatu wa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza yanaendelea kufanyika katika mitaa kadhaa ya mji mkuu Bujumbura kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.
Wakati huohuo, Jumuia ya bara ulaya imesimamisha ujumbe wake uliokuwa usimamie uchaguzi mkuu nchini Burundi.
EU inasema kuwa uamuzi huo umeafikiwa kwa sababu ya sheria kali dhidi ya vyombo vya habari, matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji, na mazingara mabaya ya vitisho kwa vyama vya upinzani.
Rais Nkurunziza anapania kuwania tena kiti cha urais kwa muhula wa tatu
Makundi ya kutetea haki za binadamu, yanasema kuwa zaidi ya watu 20 wamefariki wakati wa ghasia za maandamano.
tangu rais Pierre Nkurunziza alipotangaza mwezi uliopita kuwa anapania kuwania tena kiti cha urais kwa muhula wa tatu, kinyume na katiba ya Burundi.
Uchaguzi wa urais umepangiwa kufanyika Juni tarehe tano, huku ule wa urais ukiwa mwishoni mwa mwezi huo wa Juni.

Historia fupi ya Rais mpya wa Nigeria

Rais mpya wa Nigeria Buhari
Mshindi wa uchaguzi mkuu nchini Nigeria Muhamadu Buhari anaapishwa leo kama rais mpya wa nchi hiyo.
Bwana Buhari ambaye ni kiongozi wa zamani wa kijeshi anachukua uongozi kutoka kwa rais wa zamani Goodluck Jonathan ambaye amemtaka kuiunganisha nchi hiyo wakati inapokabiliana na tisho kutoka kundi la Boko Haram.
Buhari anasema kuwa lengo lake ni kupambana ufisadi ambao umekita mizizi katika taifa hilo lenye watu wengie zaidi barani afrika.
Lakini je Buhari ni nani ?
 
Wafuasi wa rais Buhari wakishangilia ushindi huo
Muhammadu Buhari, ni Muisilamu, mzaliwa wa Jimbo la Katsina, Nigeria kaskazini.
Alizaliwa mwaka 1942, Buhari alikuwa kiongozi wa saba wa taifa la Nigeria, baina ya mwaka 1983-1985.
Ni jenerali mstaafu aliyepata mafunzo ya kijeshi katika Nigeria, Uingereza, India, na Marekani.
Na aliwahi pia kushika nyadhifa za ugavana, kamishna wa raslimali ya mafuta, mwenyekiti wa shirika la umma la mafuta, na pia mwenyekiti wa Mfuko wa Amana ya Mafuta.
Anasemekana kuwa si m-kaishi, hakubali kushindwa.
 
Buhari alimshinda rais anayeondoka Goodluck Jonathan katika uchaguzi ulioshuhudia ushindani mkubwa
Licha ya kushindwa mara katika chaguzi tatu, amerejea kushindania tena urais, dhidi ya rais alo-madarakani Goodluck Jonathan,
Mkristo, anaye toka eneo la Niger Delta, kusini Nigeria, kwa mara ya pili, katika uchaguzi wa Machi. Unaonesha kuwa mchuano mkali.
Kuambatana na mandhari ya kisiasa, Buhari si limbukeni. Kushindwa mwaka 2003 na tena 2007, alitambia matokeo ya chaguzi hizo mahakamani bila mafanikio.
Ingawaje, Buhari anazingatiwa kuwa kiongozi mwenye ufuasi mkubwa na heshima nyumbani, hususan katika rubaa za kaskazini Nigeria.
Na hii inatokana na sera zake za kupambana na ufisadi na ukosefu wa nidhamu, wakati alipokuwa mtawala wa kijeshi.
 
Mabango ya Uchaguzi
Kimataifa, Buhari pia anasemekana kuheshimiwa.
Yajulikana kwamba ni yeye na marehemu Nelson Mandela tu ndio Wafrika binafsi waloalikwa na Ikulu ya White House, Marekani, kuhudhuria sherehe za kutawazwa Barack Obama.
Kampeni ya Jenerali Buhari, ilitilia mkazo mambo kadha, miongoni mwake utawala bora, kufufua uchumi, maendeleo ya miundombinu,
umeme na nishati, kilimo, elimu, afya, ardhi na usafiri, kuwezeshwa wanawake, usalama, na ajira. Ingawaje, uwili wa nafsi yake bado unazusha masuala, je ni wa kijeshi au kidemomkrasi?

Buhari ameapishwa kuwa rais wa Nigeria

 
Buhari ameapishwa kuwa rais wa Nigeria
Mshindi wa uchaguzi mkuu nchini Nigeria Muhamadu Buhari ameapishwa kama rais mpya wa nchi hiyo.
 
Waziri wa maswala ya kigeni wa Marekani akiwa Abuja
Bwana Buhari ambaye ni kiongozi wa zamani wa kijeshi amechukua uongozi kutoka kwa rais wa zamani Goodluck Jonathan ambaye amemtaka kuiunganisha nchi hiyo wakati inapokabiliana na tisho kutoka kundi la Boko Haram.

Kiongozi wa Ethiopia akiwasili Abuja
Buhari anasema kuwa lengo lake ni kupambana ufisadi ambao umekita mizizi katika taifa hilo lenye watu wengie zaidi barabi Afrika.
 
Wasanii wakiwatumbuiza wageni
maelfu ya mashabiki na wafuasi wake walishangilia Jenerali huyo mtaafu alipokula kiapo cha kulinda nchi hiyo.

Waandishi wa habari
Hii ndiyo mara ya kwanza kwa kiongozi wa upinzani kumshinda rais aliyeko madarakani.
Viongozi kutoka mataifa mengi duniani wakiongozwa na waziri wa maswala ya kigeni wa Marekani John kerry , rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma miongoni mwa wengine wengi.
 
Rais Buhari akikagua guaride la heshima
Muhammadu Buhari, ni Muisilamu, mzaliwa wa Jimbo la Katsina, Nigeria kaskazini.
Alizaliwa mwaka 1942, Buhari alikuwa kiongozi wa saba wa taifa la Nigeria, baina ya mwaka 1983-1985.
 
Msanii akinasa kumbukumbu ya leo
Ni jenerali mstaafu aliyepata mafunzo ya kijeshi katika Nigeria, Uingereza, India, na Marekani.
Na aliwahi pia kushika nyadhifa za ugavana, kamishna wa raslimali ya mafuta, mwenyekiti wa shirika la umma la mafuta, na pia mwenyekiti wa Mfuko wa Amana ya Mafuta.
 
Familia ya rais Buhari
Anasemekana kuwa si m-kaishi, hakubali kushindwa.
Licha ya kushindwa mara katika chaguzi tatu, amerejea kushindania tena urais, dhidi ya rais alo-madarakani Goodluck Jonathan,
 
Maafisa wa kijeshi
Mkristo, anaye toka eneo la Niger Delta, kusini Nigeria, kwa mara ya pili, katika uchaguzi wa Machi. Unaonesha kuwa mchuano mkali.
Kuambatana na mandhari ya kisiasa, Buhari si limbukeni. Kushindwa mwaka 2003 na tena 2007, alitambia matokeo ya chaguzi hizo mahakamani bila mafanikio.
 
Waageni waalikwa
Ingawaje, Buhari anazingatiwa kuwa kiongozi mwenye ufuasi mkubwa na heshima nyumbani, hususan katika rubaa za kaskazini Nigeria.
Na hii inatokana na sera zake za kupambana na ufisadi na ukosefu wa nidhamu, wakati alipokuwa mtawala wa kijeshi.
 
Awali wageni walilazimika kupiga foleni kubwa kabla ya kuingia uwanjani
Kimataifa, Buhari pia anasemekana kuheshimiwa.
Yajulikana kwamba ni yeye na marehemu Nelson Mandela tu ndio Wafrika binafsi waloalikwa na Ikulu ya White House, Marekani, kuhudhuria sherehe za kutawazwa Barack Obama.
Kampeni ya Jenerali Buhari, ilitilia mkazo mambo kadha, miongoni mwake utawala bora, kufufua uchumi, maendeleo ya miundombinu,
umeme na nishati, kilimo, elimu, afya, ardhi na usafiri, kuwezeshwa wanawake, usalama, na ajira. Ingawaje, uwili wa nafsi yake bado unazusha masuala, je ni wa kijeshi au kidemomkrasi?

ATCL yaongeza safari zake visiwa vya Comoro.



  Abiria wakishuka kwenye  Ndege ya Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL) aina ya CRJ 100. Picha ya Maktaba

SHIRIKA la ndege la taifa (ATCL) limetangaza  uamuzi wake wa kuongeza idadi ya safari zake kuelekea visiwa vya Comoro hatua inayolenga kuendana  na ongezeko la mahitaji ya huduma za shirika hilo hususani katika kuelekea kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kwa sasa shirika hilo linatoa huduma zake kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma na Mtwara kila siku. Sambamba na kutoa huduma hizo hapa nchini, shirika hilo lina mpango mpya utakaoanza rasmi tarehe mosi ya mwezi Juni mwaka huu kwa kuongeza safari zake kuelekea visiwa vya Comoro hadi kufikia mara nane kwa wiki ikiwemo mara mbili siku za Alhamisi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Bw. Johnson Mfinanga alisema shirika hilo ndilo pekee linalotoa huduma ya safari za anga kati ya Tanzania na Visiwa vya Comoro huku akibainisha fursa za kibiashara zilizopo kati ya nchi hizi mbili jambo linalosababisha uwepo wa ongezeko la mahitaji ya huduma za ATCL.

Pia amewaasa watanzania hususan wakazi wa mtwara kuchangamkia fursa hizo kwa kuwa shirika hilo kwa sasa linatoa huduma zake kati ya Mtwara na visiwa vya Comoro kwa siku za Jumatano na Ijumaa kila wiki.
“Siku zote tumekuwa tukihakikisha kwamba tunabadilika kuendana na mahitaji ya wateja wetu.

 Ni dhahiri kwamba katika kipindi hiki kuna hitaji kubwa la usafiri wa anga kuelekea visiwa vya Comoro kwa sababu za  kibiashara, mapumziko na sherehe mbalimbali, hivyo ATCL imejipanga kuchangamkia fursa hiyo,’’ alibainisha.

Akizungumzia ufanisi wa shirika hilo katika safari nyingine ikiwemo zile za Kigoma na Mtwara, Bw. Mfinanga alisema wamekuwa wakihudumia idadi kubwa ya abiria kutokana na ndege za shirika hilo kusafiri kwa mwendo kasi wa kuridhisha sambamba na huduma nzuri zinazotolewa kwa wateja wakati wa safari.
“Zaidi tunaamini kwamba huduma tunazozitoa kati ya Tanzania na Comoro zimekuwa zikichangia kuongeza ushirikiano baina ya nchi hizi mbili na tunaamini kuwa hata hili ongezeko la safari zetu kwenye mataifa haya mawili zitatoa fursa kwa wateja wetu kufaidi fursa zinazopatikana ndani ya nchi hizi,’’ aliongeza Bw. Mfinanga.

Kuhusu mpango wa shirika hilo kujipanua zaidi kihuduma, Bw. Mfinanga alisema:  “Ndege yetu aina ya De-Havilland Dash 8 Q300 kwa sasa inafanyiwa marekebisho makubwa kwenye karakana yetu iliyopo kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa  wa Julius Nyerere (JNIA) na itakapokamilika tutaendelea na huduma zetu katika mikoa ya Mwanza, Tabora, Kilimanjaro na Mbeya,’’

Bw. Mfinanga aliongeza kuwa kwa kufanya safari zake kuelekea visiwa hivyo shirika hilo limekuwa likiwezesha wateja wake kunufaika na fursa zilizopo kwenye visiwa hivyo huku pia akitoa wito kwa watanzania wengine kujitokeza kushiriki katika kuchangamkia fursa hizo.