Na Gurian Adolf
Sumbawanga
SERIKALI imeiagiza mamraka ya viwanja vya ndege nchini TAA
kuwakamata na kawachukulia hatua wananchi wenye tabia ya kukatisha katika
viwanja vya ndege kwa miguu ama kwa kutumia vyombo vya usafiri ili kukomesha
tabia hiyo.
Naibu waziri wa ujenzi na uchukuzi anayeshughulikia
usafirishaji na mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye alitoa agizo hilo jana
wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani humo ambapo pia alikagua
uwanja wa ndege wa mjini Sumbawanga ambao hauna uzio na baadhi ya watu wamekuwa
wakikatisha kati kati ya uwanja huo.
Alisema kuwa kumekuwa na tabia kwa baadhi ya watu kukatisha
katika viwanja mbalimbali vya ndege vya mikoani ikiwemo cha Sumbawanga mjini
ambapo baadhi ya wananchi wamekuwa wakikatisha kwa miguu,baiskeli,bodaboda na
bajaji kitendo ambacho ni hatari kwao na kwa wasafiri wanaotumia viwanja
hivyo.
Waziri Ntitiye pia
aliiagiza mamlaka ya viwanja vya ndege nchi kuhakikisha kuwa inaweka
uzio kuzunguka viwanja vya ndege ambavyo vipo wazi ili kuepusha madhara
yanayoweza kutokea kutokana na hali hiyo.
Pia Waziri huyo alizitaka mamlaka husika kutumia sheria
ambayo inatoa adhabu kwa watu wanaokatisha katika viwanja hivyo ambapo alisema
kuwa mtuhumiwa anatakaye bainika kutenda kosa hilo adhabu yake ni kulipa dola
200 au kifungo cha miezi sita ama vyote pamoja.
Awali kabla ya kukagua uwanja huo ambao umetengewa na
serikali fedha kiasi cha shilingi
bilioni 55.5 kwaajili ya kuujenga kisasa,waziri huyo alikutana na wawakilishi
wa wanachi ambao wana nyumba kando ya uwanja huo ambao waliiomba serikali
iwalipe fidia kwani imekuwa ni muda mrefu.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi hao mwenyekiti wanaodai
fidia hao Adrian Macheta alimwambia waziri kuwa imekuwa ni muda mrefu
wakisubiri kulipwa fidia ili kupisha upanuzi wa uwanja huo wa ndege ambapo
wanashindwa kukarabati nyumba zao na hivyo kuishi katika makazi chakavu ambayo
ni hatari kwao.
Alisema kuwa ni zaidi ya kipindi cha miaka mitano hivi sasa
hawanafaida na nyumba zao kwani baadhi yao wanakabiliwa na hali ngumu ya
kimaisha ambapo wangetumia nyumba hizo kuziweka dhamana katika mabenki na
tasisi nyingine za kifedha na kupata mikopo lakini wanashindwa kwakuwa
zitabomolewa kupita upanuzi wa uwanja huo.
Naye Joseph Nyahende mkurugenzi wa viwanja vya ndege mikoani
aliwataka wananchi kuheshimu sheria kwani kitendo cha kukatisha kinahatarisha
usalama wao na watumiaji wa viwanja hivyo ambapo aliahidi kutekeleza agizo la
waziri huyo la kujenga uzio katika viwanja vyote vya ndege nchini ambavyo
wananchi wanakatisha katikati.
Mwisho
No comments:
Post a Comment