Wednesday 14 February 2018

Mkoa watoa siku 14

Na Gurian Adolf
Katavi

SERIKALI mkoani Katavi imetoa siku 14 kwa makampuni na wafanyabiashara ambao walichukua fedha kwaajili ya kuwauzia mashine za EFDs wafanyabishara na mpaka sasa hawajui hatma ya fedha zao.
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Lllian  Matinga alitoa siku hizojana  katika kikao maalumu cha kusikiliza kero za wafanyabiashara wa mkoa huo alipo mwakilisha mkuu wa mkoa huo Meja jenerali  Mstaafu  Raphae Muhuga.
Alisema kuwa amefikia uamuzi huo baada ya kuwepo kwa makampuni ambayo yalikuwa yakikusanya fedha kutoka kwa wafanyabiashara na kuahidi kuwapelekea mashine za EFDs lakini imekuwa ni tofauti.
Matiagi alisema kuwa kutokana na kuwa wafanyabiashara hao hawajui hatma ya fedha zao na mpaka sasa hawajapata mashine hizo hivyo ameamua kutoa siku hizo warudishiwe fedha zao vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa.
''natoa siku 14 kwa makampuni yote ambayo yamechukua fedha kutoka kwa wafanyabiashara wa mkuoa huu kuhakikisha kuwa wanarudisha fedha hizo haraka iwezekanavyo tofauti na hivyo serikali ya mkoa haitasita kuchukua hatua'' alisema
Awali katika kikao hicho mwenyekiti wa wafanyabiashara wa mkoa huo Hasanaal  Dalla alimwambia mkuu huyo wa wilaya kuwa wafanyabiashara wa mkoa huo wametapeliwa na makampuni ambapo yamechukua fedha zao kwa ahadi kuwa watawaletea mashine za EFDs lakini imekuwa ni tofauti.
Alisema kuwa imepita muda mrefu mpaka hivi sasa fedha za wafanyabiashara zimechukuliwa na hawajui hatma yao ni nini hivyo alimuomba mkuu huyo wa wilaya aweze kuwasaidia.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa baadhi ya wafanyabiashara wanaonekana kana kwamba hawatii agizo la serikali la kuwataka watumie mashine hizo lakini ukweli ni kwamba walikwisha lipa fedha ili wapate mashine hizo lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea.

Mwisho

No comments:

Post a Comment