Wednesday 31 May 2017

Vijana washauriwa kuacha pombe

Na Gurian  Adolf
Sumbawanga

BAADA ya serikali kupiga marufuku pombe aina ya viroba sasa vijana mkoani Rukwa wamehamia kunywa pombe inayoitwa WIN VODKA ambayo inahifadhiwa kwenye vichupa vya plastiki na inaingizwa nchini inayoonekana inatengenezwa nchini Malawi.

Pombe hiyo imechukua  umaarufu mkubwa kutokana na kuuzwa kwa bei ya shilingi 1,200 ambapo  ina ujazo wa mililita 200,na kiwango cha ulevi asilimi 42 ambayo vijana wengi  wakiwemo wanafunzi ndiyo wanatumia sana kilevi hicho.
Gazeti hili likifanya mazungumzo na baadhi ya vijana wanaotumia  kilevi hicho walisema kuwa wameamua kuanza kutumia kwakua kinauzwa kwa bei  naafuu na kinapatikana katika maeneo mbalimbali ya kuuzia vilevi.
Mmoja wa kijana huyo  Francis Januari alisema kuwa kwasasa imekuwa  ni ngumu kupata viroba na badala yake wameamua kunywa pombe aina ya Win Vodka ambayo imepata  umaarufu kwakua bei  yake ni chini  ya kiroba ambapo kabla ya kupigwa  marufuku viroba vya konyagi vilikuwa vikiuzwa kwa bei  ya shilingi 1,500.
Mwandishi wa gazeti hili alipita mtaani na kukuta kuna  mwanafunzi mmoja akilaumiwa na wenzake kuwa ameshindwa kuhudhuria shule baada ya kulewa  pombe aina ya Win Vodka na majirani wa mtoto huyo  walisema kuwa wanafunzi wengi  wanakunywa  pombe hiyo na kushindwa kuhudhuria vizuri shuleni. 

Hata hivyo gazeti hili likiweza kuwasiliana na mganga Mkuu wa hospitali ya mkoa  wa Rukwa Emmanuel Mtika ambapo alisema kuwa pombe daima huwa siyo sawa kwa matumizi ya afya ya binadamu bila kujali kiwango cha ulevi wala wapi inatengenezwa.

Alisema kuwa katika nchi yetu kuna  tasisi kama TBS pamoja na TFDA ambazo ndizo  zinajukumu la  kuhakiki  ubora na usalama  wa vyakula  na dawa kwa watumiaji  wa  hapa nchini na nivizuri  kuhakikisha wanatumia bidhaa ambazo zimethibitishwa na tasisi hizo.
Hata hivyo baada ya kufanya uchunguzi katika kifungashio cha pombe hiyo ya WIN VODKA ilibainika kuwa hakuna muhuri wa TBS wala TFDA ili kuthibitisha kuwa wamekihakiki kilevi hicho na iwapo kinafaa kwa matumizi hapa nchini.

Mwisho

Magazeti ya Mei 31






























Tuesday 30 May 2017

Polisi Sumbawanga ashikiliwa kwa kuua

Na Gurian  Adolf
Sumbawanga

JESHI la  polisi mkoani Rukwa linamshikilia askali polisi wake anayefahamika kwa jina la  Prudence Michael  kwa kosa la  kuendesha gari kwa uzembe na kumgonga mtoto Brighton Apollo(3) na kumsababishia kifo chake.

Kamanda wa polisi mkoa  wa Rukwa George Kyando alisema kuwa kitendo cha kumgonga mtoto huyo  kilisababishwa na uzembe wa dereva barabarani kwani anapaswa kuwa makini  kwakua barabara  inatumika na watu wazima, watoto na viumbe wengine.

Tukio hilo lilitokea jana  Mei 29 majira ya saa  11 za jioni wakati polisi huyo  akiwa anaendesha gari la  jeshi  hilo maeneo ya jangwani ambapo alimgonga mtoto huyo.

Alisema kuwa kufuatia tukio hilo polisi inamshikilia askari huyo  na anatarajiwa kufikishwa mahakamani kutokana na tukio hilo.

Aidha Kamanda Kyando alitoa wito kwa madereva kuwa makini  pindi  wawapo barabarani wanaendesha vyombo vya moto ili kuepuka ajali za kugonga  ama kusababisha uharibifu wa Mali kwa kugonga  au hata wao wenyewe usalama  wao kwakua ajali inapotokea inasababisha madhara makubwa.

Hata hivyo alitoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba huo na kuendelea kusisitiza umakini kwa watumia Barabara kwa madereva pamoja na watembea kwa miguu kwani yeye binafsi na  jeshi hilo wanasikitishwa kutokana na ajali hizo.
 
Mwisho

Msipokee wageni mtasababisha Ebola

Na Gurian Adolf
Sumbawanga

KUTOKANA na kuwepo kwa ugonjwa wa ebola katika nchi Jirani ya Kidemokrasia ya Kongo DRC mkoa wa Rukwa unapaswa kudhibiti watu wananoingia na kutoka katika nchi hiyo kwa kutumia njia za panya ili wasisababishe kuingia nchini virusi vya ugonjwa  huo.

Akizungumza na wananchi wa mji wa Kirando wilayani Nkasi mkoani Rukwa mkuu wa mkoa huo Zelote Steven alisema kuwa mpaka sasa hakuna mgonjwa wala dalili isipokuwa ni tahadhari na elimu inaendelea kutolewa kwa wananchi wa mkoa huo ambao baadhi ya maeneo yake yanapakana na nchi ya Kongo ambayo tayari imeripotiwa kuwepo kwa ugonjwa wa Ebola.

Gazeti hili lilifanya jitihada ya kuzungumza na wakazi wa maeneo ambayo ndiyo imekuwa njia za panya ambazo wananchi wa nchi za Tanzania na Demokrasia ya Kongo DRC wamekuwa wakizitumia kuingia na kutoka na iwapo serikali itaziwekea ulinzi madhubuti huenza zikasaidia kukabiliana na tishio la ugonjwa huo kuingia hapa nchini.

Akizungumza na gazeti hili mmoja wakazi wa kijiji cha Kirando Matayo Ntiha aliyataja maeneo ambayo hutumika na wananchi wa nchi hizi mbili kuingia na kutoka kuwa ni maeneo ya kijiji hicho cha Kirando Kalungu Mvuna Namasi Kazovu Kaolongwe Kampemba Utinta Pamoja Na Kabwe.

Alisema kuwa kutokana na historia nzuri  ya ujirani mwema, udugu kupendana na kuoana watu kutoka katika nchi hizi mbili wamekuwa wakitembeleana kwa lengo la kusalimiana sambamba na kufanya biashara hali ambayo imezoeleka kutokana na kutokuwa na hila mbaya kutoka upande wowote kwakua wamekuwa wakiishi kama ndugu na wakitambua kuwa wote ni waafrika hivyo wamekuwa wakiishi kwa misingi  ya kupendana na kujaliana.

Alisema kuwa wananchi kutoka katika nchi ya Kongo wamekuwa wakiingia humu nchini kwa njia halali na haramu kwalengo la kufanya biashara kutembelea ndugu jamaa na marafiki hali kadharika kutoka nchini kwetu Tanzania na kwenda katika nchi hiyo kwa lengo hilo lakini hali imebadirika kutokana na kuwepo kwa ugonjwa wa Ebola hivyo sasa nivizuri serikali ikachukua hatua kudhibiti uingiaji na utokaji wa wananchi kiholela tofauti na hapo awali.

Ntiha alisema kuwa ni jukumu la serikali kupitia wataalamu mbalimbali kudhibiti hali hii iwapo kunania ya dhati ya kuzuia ugonjwa huo usiweze kuingia hapa nchini na elimu kuendelea kutolewa kwa wananchi ili waache kuwapokea wageni kutoka katika nchi hiyo ili kuepusha kuwepo mgeni ambaye anaweza kuingiza ugonjwa huo katika maeneo yao ambayo pia sehemu kubwa yanatenganishwa na ziwa Tanganyika na wakati mwingine inaweza kuwa ngumu kuwadhibiti watu wanaoingia hapa nchini kwa kulindamipaka ila  elimu dhidi ya hatari na adhari za mgonjwa huo ndio inaweza ikawa njia sahihi kwakua wananchi wanaogopa kufa kwa ugonjwa huo.

Hivi karibuni  Mkuu wa mkoa huo akiwa pamoja na Mkuu wa wilaya ya Nkasi, Said Mtanda walifanya ziara ya siku tatu kwaajili ya kuzungumza na wananchi wa maeneo hayo kwa lengo la kuwasisitiza kuacha tabia ya kupokea na kuwaficha wageni wanaoingia kinyemela nchini kwani huenda wakasababisha kuingia pia kwa ugonjwa huo ambao ni hatari na unagharimu maisha ya watu kwa kiasi kikubwa.

Hata hivyo viongozi hao waliwaahidi wananchi hao kuwa serikali imekwisha kujipanga kwaajili ya kukabiliana na ugonjwa  huo ni wao kuhakikisha wanafuata maelekezo kutoka kwa wataalamu na wapunguze sana kukimbilia katika tiba za jadi  kwani mengi ya magonjwa  hayatibiki huko isipokuwa sayansi tu kupitia hospitali ndiyo inatoa ufumbuzi wa matatizohayo na ndiyo sababu serikali ya awamu ya tano  inatenga bajeti kubwa katika wizara ya afya ili wananchi waweze kuudumiwa kupitia huduma za afya za kisasa.

Mwisho

Magazeti ya Mei 30