Thursday 8 June 2017

Mtangazaji wa zamani afariki dunia

Na Walter  Mguluchuma
Katavi

MTANGAZAJI wa zamani wa Radio Tanzania Dar es salaam(RTD) ambayo hivi sasa inafahamika kuwa ni Shirika la utangazaji la Taifa(TBC),Lucas Matipa (77) amefariki Dunia akiwa nyumbani kwao Wilayani Mpanda Mkoani Katavi alikokuwa akipatiwa matibabu.


Kwa mujibu wa kaka wa marehemu huyo Padri Simoni Matipa alisema Lucas alifariki jana majira ya saa 12:30 asubuhi nyumbani kwao katika Mtaa wa Majengo Manispaa ya Mpanda.

Padre Matipa alisema marehemu alizaliwa mwaka 1940 huko Tarafa ya Karema Wilayani Mpanda kwa sasa Wilaya ya Tanganyika na alisitaafu kazi ya uandishi wa Habari na utangazaji wa Radio Tanzania mwaka 2006.

Enzi za uhai wake marehemu alifanya kazi na wandishi wa habari na watangazaji mbalimbali hapa nchini.

Alisema marehemu Lucas Matipa alianza kusumbuliwa na maradhi toka mwaka juzi hali ambayo ilimlazimu atoke jijinj Dares salaam alikokua akiishi na kurudi nyumbani kwao Mpanda .

Ibada ya mazishi ilifanyika jana katika kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda na ibada hiyo iliongozwa na Paroko Msaidizi wa Kanisa hilo Padri Dominick Odiyambo aliyeshirikiana na Padri Simoni Matipa.

Wakati wa misa hiyo ya mazishi Padri Odyambo alieleza kuwa marehemu Lucas Matipa wakati wa uhai wake alifanya kazi vizuri ya uandishi wa habari na utangazaji vizuri .

Alsema kutokana na utendaji wake mzuri wa kazi ya uandishi wa habari ndio maana Taifa lilimwamini na yeye alibahatika kuzungumza nae mara kwa mara katika kipindi cha hivi karibuni na alikuwa akimwelezea jinsi alivyofanya kazi ya uhandishi wa habati hapa nchini na nje ya nchi kabla ya kustaafu kwake mwaka 2006.

Mazishi ya marehemu Lucas Matipa yalifanyika jana katika makaburi ya Mwangaza na yalihudhuliwa na mami ya wakazi wa mji wa Mpanda na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Katavi Mselemu Abdalla na Meya wa Manispaa ya Mpanda Willy Mbogo.Mwisho

No comments:

Post a Comment