Monday 12 February 2018

UWT Rukwa yachagua kamati ya utekelezaji

Na Gurian Adolf
Sumbawanga
WAJUMBE waliochaguliwa katika nafasi ya utekelezaji ya umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi UWT  mkoa wa Rukwa wametakiwa kuachana na dhana kuwa katika nafasi hiyo watafanikiwa kiuchumi kwani kazi yao kubwa wapon kwaajili ya kujitolea kwa maslahi ya chama.
Mwenyekiti wa umoja huo Merry  Kalula aliyasema hayo jana wakati akifunga baraza maalumu la UWT mkoa lililoketi katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga kwaajili ya kuwachagua wajumbe wanaounda kamati ya utekelezaji wa umoja huo.
Alisema kuwa iwapo kuna mjumbe amegombea nafasi ya ujumbe wa utekelezaji kwa nia ya kutafuta mashahi ni vizuri akajiuzuru ili nafasi yake ikajazwa na mjumbe mwingine kwani kazi inayofanywa ni kujitolewa na wala si kutafuta kipato.
Kalula alisema kuwa sehemu kubwa ya chama hicho wanajitolea,hakuna maslahi yoyote ya kiuchumi wanayoyapata na wanawajibika kukipigania chama hicho ili kiendelee kushika dola ndiyo lengo kubwa la umoja huo na chama cha mapinduzi kwa ujumla.
‘’napenda niwaambie wajumbe mliochaguliwa,kama kunamwanachama aligombea kwaajili ya kutafuta maslahi ya kiuchumi ni vizuri akaachia ngazi kwakua sehemu kubwa tunajitolewa asiwepo mjumbe ambaye amefuata maslahi’’ alisema.
Alisema kuwa UWT mkoa inajukumu kubwa la kuhakikisha kuwa chama hicho kinashinda chaguzi mbalimbali zinazotarajiwa kufanyika na kila mwanajumuia hiyo anapaswa kutambua anafanya jitihada ya kuongeza wanachama waaminifu watakao kuwa wakikichagua chama cha mapinduzi.
Awali akimkaribisha mwenyekiti wa umoja huo katibu wa UWT mkoa Aziza Kiduda alisema kuwa taratibu zote zimefuatwa na wagombea nane wlijitokeza katika kuwania nafasi tano zinazounda kamati ya utekelezaji ya jumuia hiyo.
Waliochaguliwa ni wajumbe wa baraza mkoa wa UWT ambao ndio walipaswa kuwa wagombea wa nafasi ya kamati ya utekelezaji kwa mujibu wa katiba ya umeoja huo.
Mwenyekiti wa umoja huo alimtangaza Ester Wafulukwizya,Rose Chilumba,Mariam Seleman,Rehema Kauzeni pamoja na Mariam Meghji kuwa ndio walioshinda katika uchaguzi huo na kuwa watakuwa wajumbe wa kamati hiyo kwa miaka mitano ijayo.
Akitoa shukrani kwa wapiga kura mmoja wa washindi Ester Wafulukwizya aliwashukuru wajumbe kwa imani kubwa kwa kuwachagua,na pia aliwasihi wale ambao hawakuchagulia wasijioni kuwa hawafai kwani nafasi zilikuwa tano na wagombea ni wanane hivyo lazima wengine wangekosa nafasi.
Alisema kuwa kilichopo ni kushikamana ili kukijenga chama hicho kwani kila mmoja anawajibika kuhakikisha CCM inapata ushindi lakini kama watajitokeza wa kuanzisha mivutano itasababisha kudhoofisha ushindi wa chama hicho katika chaguzi mbalimbali zijazo.
Mwisho  

3 comments: