Saturday 24 February 2018

Serikali ya mkoa yataka mkandarasi alipwe haraka ili amalize ujenzi wa barabra

Na Gurian Adolf
Kalambo

SERIKALI mkoani Rukwa imeshauri mwanamuziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul  (Diamond) atumike kuyatangaza maporomoko ya Kalambo Falls yaliyopo mpakani mwa nchi ya Zambia na Tanzania katika kijiji cha Kapozwa wilaya ya Kalambo mkoani humo.
Mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo alitoa ushauri huo juzi wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi na aliyatembelea maporomoko hayo ambayo ni yapili kwa urefu barani Afrika yenye urefu wa kina zaidi ya mita 230 kwenda chini.
Alisema kuwa maporomoko hayo bado hayajatangazwa vya kutosha kwani watu wengi ikiwemo watanzania wenyewe hawayajui hivyo ili yaweze kufahamika nilazima yakatangazwa na mtu ambaye anafanya vizuri katika sanaa ambaye yeye binafsi anao Diamond anafaa kufanya kazi hiyo.
Wangabo alisema kuwa maporomoko hayo ni miongoni mwa fursa za kitalii mkoani humo ambapo zikitangazwa vizuri zitasababisha kuongeza kipato katika wilaya ya Kalambo,mkoa wa Rukwa na nchini kwa ujumla.
Alisema kuwa mikakati ifanyike ili kujua hatua gani zifikiwe ili Diamond apewe kazi hiyo kwani ni wajibu wa watanzania waliofanikiwa kutangaza rasilimali zao kwani mapato yanayopatikana yanainufaisha nchi kwakuwa watakao tembelea ni watalii wa ndani pamoja na nje ya nchi.

Akizungumzia kauli hiyo ya mkuu wa mkoa mmoja wa wakazi wa kijiji cha Kapozwa wilayani Kalambo ambapo yapo maporomoko yako John Simtowe alisema kuwa anamshukuru mkuu huyo wa mkoa wa Rukwa Wangabo kwa uamuzi wa kuyatangaza maporomoko hayo kwani alisema kuwa iwapo yatafahamika na watalii kuanza kuyatembelea watanufaika kiuchumi.
Alisema kuwa maporomoko ya Kalambo kuwepo katika kijiji hicho ni fursa kwao kwakuwa watafanya biashara kwa watalii watakao kuwa wanayatembelea na kupata fedha tofauti na hivi sasa ambapo hawapati fedha licha ya kuwepo kwa utajiri huo mkubwa ambao bado hauja tangazwa ipasavyo.
Mwisho

No comments:

Post a Comment