Sunday 25 February 2018

Serikali haina mpango wa kuwakopesha wachimbaji wadogo

Na Walter Mguluchuma
Katavi

SERIKALI
imesema kuwa   haina  mpango  wa  kuwakopesha fedha wachimbaji wadogo  bali imeahidi kutatoa mikopo wa vifaa baada ya kubaini kuwa fedha  zilizokuwa  zikitolewa awali wachimbaji hao zilikuwa  hazitumiki kama  ilivyokusudiwa.

Naibi  Waziri wa madini   Doto  Biteko aliyasema hayo jana wakati alipokuwa  akiwahutubia  wachimbaji wadogo wa  madini wa  mkoa wa  Katavi  katika  mkutano wa   hadhara uliofanyika katika   machimbo ya  dhahabu ya   Ibindi  Wilayani   Mpanda.


Alisema  kuwa  Wizara ya  madini imeamua kuondoa  utaratibu  wa  hapo  awali  wa kuwakopesha  fedha wachimbaji wadogo kwa  ajiri ya kununulia  vifaa  vya  kufanyia   shughuli za uchimbaji  na   badala  yake watakuwa  wanawakopesha vifaa.
Waziri huyo alisema kuwa   fedha  zilizokuwa  zikitolewa  na  Serikali  kwa   ajiri ya kuwakopesha  wachimbaji   wadogo  zimekuwa    hazitumiki  kama  ilivyokusudiwa  na   badala  yake wamekuwa  wakizitumia kwa  matumizi       mengine.
 Alieleza  wachimbaji  wadogo  wamekuwa  wakikopeshwa   fedha  kati ya  shilingi Milioni 100 na  milioni 200   lakini  badala ya  kununua  vifaa  vya  kuchimbia    madini wao wamekuwa wakizitumia kwa  ajiri ya  kununua  magari na  kujengea   nyumba .
  Alisema  kuwa     wachimbaji  wadogo  wote  walikopeshwa   fedha  na   wakashindwa  kuzirudisha  wanatakiwa  wazirudishe   mara  moja  kwani kwa  wale watakao shindwa  kurejesha watakamatwa  na  kufikishwa   mahakamani .
  Aliwataka  wachimbaji  wote wa  madini   hapa   nchini    wawe  waaminifu  kwenye  kulipa   kodi  za   Serikali na  wachimbaji  wadogo waache  tabia yao ya  vichochoro   vya  kusafirisha   madini kwa  njia ya  magendo kwani  mchango wa  sekta ya  madini   bado ni  mdogo  kwenye   mapato ya  Taifa  kutoka  na  madini  mengi kuzushwa  nje ya  nchi .
Alisema   Serikali  haiko   tayari  kuona  kazi  zinazoweza  kufanywa  na   Wanzania  kwenye  migodi ya   madini  zinafanywa  na  watu wa kutoka  nchi za   nje  kwani lengo la  Serikali ni kutaka kuona   Watanzania  wananufaika   na  rasilimali za  madini .
Mwenyekiti wa   Chama  cha  Wachimbaji wadogo wa  Mkoa wa  Katavi  Willy  Mbogo   aliiomba  Wizara ya     madini  kutunga   sheria    ambazo   zitakuwa   zinawapa  nafuu   kwani   sheria  za  sasa  haziangalia   aina ya  wachimbaji  wadogo  na wakubwa .
  Alisema   yapo  maeneo  ambayo  ambayo   baadhi ya  wachimbaji  wanayamiliki kwa  kuwa  na  leseni  lakini  yamekuwa  hayaendelezwi  hivyo   ni   vema   serikali   ikawafutia   leseni  wachimbaji  hao .
Katibu  wa  chama  wa   wachimbaji  wadogo wa  Mkoa  huu   Filberti   Sanga   aliomba  wizara  ya  madini  iwafutie  leseni  wachimbaji   ambao     wachindwa  kuyaendeleza  na  bbadala yake  wapewe wachimbaji  wadogo .
 Alisema  wapo  wamiliki wa  leseni  za  madini    ambao  maeneo yao  hawayaendelezi wamekuwa  wakibadili  majina  kila  muda  wao  wa  leseni  kumalizika  kwa kuhofia  kufutiwa  leseni zao .
Mwisho

No comments:

Post a Comment