Wednesday 21 February 2018

Wafugaji lawamani kukabili mimba za utotoni

Na Gurian Adolf
Nkasi

BAADHI ya wafugaji wilayani Nkasi mkoani Rukwa wamelaumiwa kwakuwa ni kikwazo cha sheria kuchukua mkondo wake katika jitihada za kupambana na mimba za utotoni.
Akizungumza hivi karibuni  mwenyekiti wa kijiji cha Mtenga Soatenes Kalikwenda katika kikao cha siku moja kilichofanyika katika hicho na kufadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Plan International chenye lengo la kupitia utekelezaji wa mradi wa kupambana nandoa pamoja na mimba za utotoni mwaka 2017 na kuandaa mpango mkakati wa mwaka 2018.
Alisema kuwa baadhi ya wahusika katika kesi hizo wanakuwa ni watoto wa wafugaji ambao wanaishi maisha ya kuhama hama kwaajili ya kutafuta malisho ya mifugo hivyo hujikuta wakihama wakati mashauri hayo yapo mahakamani.
''unakuta aliyepewa ujauzito ni mtoto wa mfugaji,bila kujali kuwa shauri linaendelea mahakani yeye anahama na mtoto wake kwaajili ya kutafuta malisho ya mifugo matokeo yake hawafiki mahakamani na hakuna kinacho endelea'' alisema
Alisema kuwa jambo hilo limekuwa ni changamoto kubwa kiasi kwamba linafifisha jitihada za kukabiriana na ndoa za utotoni pamoja na mimba za utotoni kwakuwa wahusika wanafikiria zaidi mifugo  kuliko hata maisha ya baadae ya watoto wao kuwekeza kwenye elimu.
Naye diwani wa kata ya Mtenga Pankras Maliyatabu alisema kuwa changamoto nyingine iliyopo ni jeshi la polisi kutochukua hatua kwa wakati kitendo kinacho sababisha baadhi ya watuhumiwa kuhama ama kukimbia kabisa.

Diwani huyo alisema kuwa changamoto nyingine ni mtoto mjamzito kufundishwa akataje mahakamani mtuhumiwa zaidi ya mmoja na baada ya kufanya hivyo watuhumiwa huachiwa huru kwakuwa hakuna ujauzito ambao unawahusika wa kiume wawili.

Awali akizungumza wakati wa kupitia mpango kazi huo mratibu wa mradi wa  kuzuia mimba za utotoni wilayani humo,kutoka shirika lisilo la kiserikali la Plan International Nestory Frank alisema kuwa shirika hilo limekwisha baini michezo hiyo lakini isiwe sababu ya kuwakatisha tamaa.
Alisema kuwa kila kazi inachangamoto zake lakini pamoja na mapungufu yaliyopo mafanikio ni makubwa kuliko hapo awali hivyo wanapaswa kuandaa mikakati mipya ya kukabiliana na suala hilo kwani wanaopata madhara ni watoto hao wakike ambao baadhi yao hawajui kuwa wanachokifanya kinaharibu maisha yao ya baadaye.
Mratibu huyo aliisihi jamii wilayani humo kujiandaa kuendeleza mapambano ya tatizo hilo kwakuwa mradi huo upo katika awamu ya tatu na yamwisho na unatarajia kufikia mwisho mwakani.
 
Mwisho

No comments:

Post a Comment