Saturday 8 July 2017

OCD mstaafu ateuliwa

Na Walter Mguluchuma
Katavi
JESHI la polisi mkoani Katavi limemteua aliyekuwa OCD na  aliyestaafu hivi karibuni wa wilaya ya Mpanda mkoani humo, Zeno Malesa kuwa  mshauri wa maswala ya ulinzi na usalama wa  Mtaa wa  Kasimba  katika  Manispaa ya  Mpanda  kutokana na juhudi zake alizokuwa akizifanya za kupunguza matukio ya  ujambazi pamoja na biashara ya ukahaba kabla ya kustaafu kwake kazi katika  jeshi hilo katika wilaya hiyo.
Uamuzi  huo wa kumteuwa  Malesa kuwa   mshauri wa masuala ya ulinzi  katika mtaa   huo ulifanywa na  Kamanda wa  Polisi mkoa wa   Katavi  Damas Nyanda wakati wa sherehe za  kumuaga mstaafu huyo na zilizofanyika   katika  ukumbi wa   Neema uliko  katika   Mtaa wa  Kawajense  Manispaa ya  Mpanda.
  Alisema  OCD kuwa mstaafu  huyo amelitumikia  jeshi la polisi kwa  uaminifu  mkubwa   kuanzia  mwaka  1973 alipojiunga  na  jeshi  hilo  hadi   Julai 1  mwaka huu ambapo  ameweza  kufanya  kazi ya  polisi kwa  kipindi cha   miaka  44 kwa uadilifu mkubwa.
 Alifafanua  kuwa  kwa  kipindi   alichoongoza  Wilaya ya   Mpanda  amefanya  kazi  nyingi  mbalimbali za  kupambana  na  uharifu na  ameweza kupunguza  matukio ya ualifu   kwa kiasi kikubwa.
Pia  ameweza  kupunguza  matukio ya  biashara ya ukahaba na  matukio  kumi  kwa  kipindi cha  mwaka  jana  hadi  kufikia  matukio  matatu kwa  kipindi cha  mwaka huu   wa  2017.
Nyanda   alieleza  kuwa  kutokana  na  mchango wake huo   mkubwa   katika  jeshi la  polisi   ndio  maana   ameamua kumteuwa  kuwa  mshauri wa  maswala  ya ulinzi na   usalama  katika   mtaa  anao ishi wa   Kasimba  iliaendelee kutoa  mchango wake kwa  jeshi la  polisi.
Naye  Katibu  Tawala wa   Mkoa  wa  Katavi  Kamishna wa  Polisi  Paulo  Chagonja  alisema  kuwa jeshi la  polisi   linajivunia  mafanikio ya  OCD  huyo  mstaafu  na atakuwa  ni  daraja  kati ya  polisi na  raia na  Balozi.
 Alisema ukiona  mtumishi wa  jeshi la  polisi  ameweza kufanya kazi na kufikia   ngazi  aliyokuwa  nayo  Malesa ujue kuwa   mtu  huyo  alikuwa ni  mwadilifu  na  ndio  maana  jeshi la  polisi  lilimwamini.
Kwaupande wake mwenyekiti wa  Kamati ya  ulinzi na  usalama wa  Wilaya ya  Mpanda ambae  pia  ni   mkuu  wa   Wilaya ya   Mpanda   Lilian   Matinga   alisema kuwa   hali ya   matukio ya  uharifu kwa  wilaya ya   Mpanda   yamepungua kwa kiasi  kikubwa  kutokana na  ushirikiano  ulipo  baina ya  polisi na   wananchi  hivyo   alimtaka   ocd   aliyehamishiwa  kwenye  Wilaya  hiyo kuendeleza ushirikiano  na  mahusiano na  wananchi  kama uliokuwepo hapo awali.
Mwisho
.

No comments:

Post a Comment