Saturday 24 February 2018

Padre ashauri watoto wajawazito wafungwe

Na Walter Mguluchuma
Katavi

PADRE
wa Kanisa  Katoliki Jimbo la Mpanda mkoani Katavi, Leonald  Kasimila ameishauri serikali ya mkoa huo kuanza kuwachukulia hatua za kisheria  wasichana  wanaopata  mimba wakiwa  na  umri mdogo pamoja  na  wanaume  waliowapa ujauzito ili iwe ni njia ya kupunguza  tatizo  la  ongezeko la mimba za   utotoni katika mkoa huo.

Ushauri huo  aliotoa jana  kwenye  kikao cha kamati  ya ushauri cha mkoa wa  Katavi RCC  Kilichofanyika jana mkoani humo.

Padre Kasimila alikiambia  kikao  hicho  kuwa  mimba  za utotoni  kwa  asilimia 80  zimekuwa   zikichangiwa na wanaume  na   vijana  wa kiume  huku asilimia 20 zikisababishwa na  wasichana  wenyewe.
 Alisema  ilikukabiliana  na  tatizo  hilo  ni vizuri  sasa   ukaanzishwa  utararibu na   sheria ya kuwakamata na  kuwafungulia   mashitaka wasichana  wanaopata  mimba  badala ya  utaratibu wa  sasa wa kuwakamata wanaume  peke yao.
Aliwaeleza  wajumbe wa  kikao  hicho kuwa kitendo cha kutowachukulia  hatua wasichana  wanaopata   ujauzito  wakiwa  na  umri  mdogo  kunazidi kuwafanya  waone  jambo hilo ni kitu cha  kawaida.

Naye mbunge wa  jimbo  la   Mpanda  Vjijini  Moshi  Kakoso  alisema   kuwa   idadi ya  wanafunzi  wanaoanza kusoma  darasa   la  kwanza  na  wanaofanikiwa  kumaliza shule huwa hailingani  kwa   wanafunzi wa mkoa huo  kutokana  na   baadhi yao kupata  ujauzito wakiwa wanasoma.
 Alisema  zipo  sababu zinazosabisha  wasichana   wengi  kupata ujauzito  na  kuwafanya   wakatishe   masomo  yao kwa   wanafunzi wa   Shule  za   Msingi na   Sekondari ambapo alitaja  miongoni mwa  sababu za  kuwepo kwa  mimba  za utotoni  kuwa ni utoro uliokithiri.
Wanafunzi  kutembea  umbali   mrefu  kwenda  shule hali  ambayo  imekuwa   ikiwafanya  wasichana   kupata    vishawishi  wakati wakiwa  njiani.
Aliomba   Serikali ya   Mkoa  wa  Katavi  ihakikishe  maeneo  ambayo   hayana   vijiji   rasmi  watu wasiruhusiwe   kuishi  kwani   ndio  wamekuwa wakisababisha  watoto wao  kuwa  mbali  na  shule  wanazo  soma.
Afisa  Elimu wa   Mkoa  wa    Katavi   Ernesti   Hinju  alisema   tatizo  la   mimba  za  utotoni kwa   Mkoa wa   Katavi  lipo  na  kwa  takwimu  zilizotolewa  hivi  karibuni   Mkoa  huo   unaasilimia  45 za   mimba  za utotoni   hali  ambayo inaufanya   Mkoa  huo  kuongoza  kwa  kuwa  na  idadi kubwa za  mimba za utotoni hapa   nchini.
Alisema  mimba  hizo  zimekuwa  pia   zikitokea  kwa  wanafunzi wa  sekondari  wakati   ambao  wanapokuwa   wapo    likizo   hivyo jukumu  la  kumlinda   mtoto wa  kike  sio la   walimu  na   mzazi wa  mtoto peke yao  bali  ni  la jamii nzima.
Mkuu wa  Wilaya ya  Mlele  Rachae  Kasanda   aliwaeleza  wajumbe wa kikao  hicho  kuwa  katika   Wilaya  yake ya   Mlele    ameisha anza kuwachukulia  hatua  wazazi wa  wasichana  wanaopata ujauzito wakiwa  na  umri  mdogo .
Pia  katika   Wilaya  hiyo    wameweka    utaratibu wa  kufanya   msako  kwenye   kumbi  za    starehe  na    endapo   watamkuta  mtoto  mwenye  umri  mdogo  huwa  wanamkamata  yeye  na  wazazi  wake.
Mwisho

No comments:

Post a Comment