Na Gurian Adolf
Katavi
CHAMA cha mapinduzi CCM mkoani Katavi kimewaonya baadhi ya wanachama wake waache mara moja tabia ya kuwa andaa wanachama wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kabla ya muda kwani kitendo hicho kinasababisha uhasama baina ya wanachama na mipasuko ndani ya chama hicho.
Onyo hilo lilitolewa hivi karibuni na katibu wa chama hicho mkoa wa Katavi Kajoro Vyahoroka wakati alipokuwa akiwatubia wananchi wa Kata ya Majalila katika mkutano uliondaliwa na Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini Moshi Kakoso uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi Majalila wakati Mbunge huyo alipokuwa akikabidhi kompiyuta 25 zenye thamani ya milioni 50 kwa ajiri ya shule sita za Sekondari za jimbo hilo.
Alisema kuwa wapo baadhi ya viongozi wa chama hicho wa ngazi mbalimbali wameanza kuwapigia kampeni viongozi wanao wataka wao wakati ni kinyume na taratibu na watakao bainika hawata sita kuwachulia hatua kali za kinidhamu.
Alisisitiza kuwa ni vema viongozi walipo madarakani kwa sasa waachwe watimize wajibu wao ili wakati ukifika waje waulizwe waliokuwa wameyahidi kwa wananchi wao ndipo wanachama waone kama wanastahili kuchaguliwa tena ama laa.
Alieleza kuwa kitendo cha viongozi kuanza kuwaandaa viongozi wanao wataka wao kinawafanya viongozi walipo madarakani waanze kuvunjika moyo katika utekelezaji wa majukumu yao na kujenga chuki kwa wananchama wanaoandaliwa hali inayosababisha makundi ndani ya chama hicho.
Kwenye mkutano huo Katibu wa CCM wa Mkoa wa Katavi alipokea kadi 150 kutoka kwa wanachama wa vyama mbalimbali vya upinzani na kuwakabidhi kadi za CCM ambapo baadhi yao walimwakikishia Katibu huyo kuwa wao na wake zao kuanzia siku hiyo wamehamia rasmi CCM .
Mmoja wa wanachama hao wapya Juma Ramadhan alisema wameamua kurudi Ccm kutokana na kasi ya maendeleo ilipo sasa inayofanywa na Serikali ya awamu ya pili inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli.
Naye Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vjijini Moshi Kakoso alisema kuwa Jimbo lake na Wilaya ya Tanganyika wamepata maendeleo kwa haraka kutokana na jinsi viongozi wanavyofanya kazi kwa ushirikiano bila kuwepo na migogoro yoyote.
Alisema anamwombea heri Mkuu wa Wilaya hiyo Salehe Mhando asihamishwe kwenye Wilaya hiyo kutokana na utendaji kazi wake kwani amekuwa akifanya kazi mpaka anasahau kujenga mwili wake kwa kushindwa hata kula kwa ajiri ya majukumu ya kuwatumika wananchi .
Kwa upande wake mkurugenza wa Halmashauri hiyo Romuli Rojas alisema kuwa Wilaya hiyo imepiga hatua kubwa ya maendeleo kwenye sekta mbalimbali kama vile afya ,barabara ,mawasiliano elimu maj, na kilimo.
Mwisho