Friday 25 May 2018

viongozi wa dini waaswa

Na Gurian Adolf
Sumbawanga



VIONGOZI wa madhehebu ya Kikristu mkoani Rukwa wameshauriwa kuwaelekeza waumini wao namna bora ya kushiriki ibada ili kuepuka hofu ya kuambukizana magonjwa mbalimbali hususani nyakati hizi ambapo mkoa huo unakabiliwa na hofu ya magonjwa ya kipindupindu na Ebola.

Mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo alisema kuwa katika madhehebu ya Kikristo kunakipengele cha waumini kutakiana amani wakati wa ibada ambapo baadhi ya waumini hushikana mikono na wengine kukumbatiana hali ambayo ni hatari kwani kunawengine miili yao inakuwa inatoka jasho.

''mimi pia ni Mkristo huwa nikiwa katika ibada kunakipengele cha kutakiana amani ambapo huwa tunapeana mikono waumini,baadhi ya waumini mikono yao inakuwa na majimaji yaani jasho, na ugonjwa wa Ebola unaenezwa kwa maji maji ya mwili ikiwemo jasho hii inaweza kuwa hatari pia.

Alisema kuwa inafaa sasa viongozi wa dini waone namna bora ya kuwaelekeza waumini wao namna ya kushiriki ibada bila kuwa na hofu ya kuambukizana magonjwa mbalimbali hasa kipindu pindu kilichopo hivi sasa mkoani mkoani humo.

Akitoa taarifa katika hiivi karibuni katika kikao cha kamati ya afya ya mkoa huo ambayo ilikutana kwa lengo la kuweka mikakati ya kukabiliana na magonjwa ya Ebola pamoja na kipindu pindu mganga mkuu wa mkoa huo Bonifas Kasululu alisema kuwa pamoja na nchi jirani ya Kidemokrasia ya Kongo kukabiliwa na ugonjwa wa Ebola lakini katika mkoa wa Rukwa hakuna hofu yoyote.

Alisema kuwa mpaka hivi sasa kusiwepo hofu yoyote kwa wananchi na maisha yanapaswa kuendelea kama kawaida iwapo kutakuwa na tishio hilo idara ya afya iko makini na inafuatilia kwa umakini kila hatua na itatoa taarifa iwapo kuna mtu amebainika kuwa na dalili za ugonjwa huo.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment