Monday 28 May 2018

CCM yawaonya wanachama wake

Na Gurian Adolf
Katavi

CHAMA cha mapinduzi CCM mkoani Katavi kimewaonya baadhi ya wanachama wake waache mara moja tabia ya kuwa andaa wanachama wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kabla ya muda kwani kitendo hicho kinasababisha uhasama baina ya wanachama na mipasuko ndani ya chama hicho.

Onyo  hilo lilitolewa hivi karibuni na katibu wa chama hicho mkoa wa Katavi Kajoro  Vyahoroka wakati  alipokuwa akiwatubia  wananchi wa   Kata  ya  Majalila katika mkutano uliondaliwa na  Mbunge wa  Jimbo la  Mpanda   Vijijini  Moshi  Kakoso uliofanyika  kwenye   uwanja wa  shule ya  Msingi  Majalila wakati  Mbunge  huyo  alipokuwa  akikabidhi  kompiyuta 25   zenye  thamani ya  milioni 50 kwa  ajiri ya  shule  sita za  Sekondari  za  jimbo hilo.

Alisema kuwa wapo baadhi ya  viongozi wa  chama   hicho wa  ngazi mbalimbali  wameanza kuwapigia kampeni viongozi  wanao wataka wao  wakati ni kinyume  na taratibu na  watakao  bainika  hawata  sita  kuwachulia  hatua  kali za  kinidhamu. 

 Alisisitiza kuwa  ni  vema  viongozi  walipo  madarakani  kwa  sasa  waachwe  watimize  wajibu wao  ili  wakati ukifika  waje waulizwe  waliokuwa  wameyahidi kwa  wananchi  wao ndipo wanachama waone kama wanastahili kuchaguliwa tena ama laa.
 Alieleza  kuwa  kitendo  cha viongozi kuanza kuwaandaa  viongozi  wanao wataka wao kinawafanya viongozi walipo  madarakani  waanze kuvunjika  moyo  katika  utekelezaji wa majukumu  yao na kujenga chuki kwa wananchama wanaoandaliwa hali inayosababisha makundi ndani ya chama hicho.
 Kwenye  mkutano huo  Katibu wa  CCM  wa  Mkoa wa  Katavi  alipokea  kadi    150 kutoka   kwa  wanachama wa  vyama  mbalimbali vya upinzani na  kuwakabidhi kadi za   CCM  ambapo  baadhi yao walimwakikishia  Katibu  huyo kuwa  wao na  wake  zao  kuanzia  siku  hiyo  wamehamia rasmi  CCM .
Mmoja  wa  wanachama  hao wapya    Juma    Ramadhan alisema  wameamua  kurudi    Ccm kutokana  na  kasi ya  maendeleo  ilipo  sasa   inayofanywa na  Serikali ya  awamu ya  pili inayoongozwa na  Rais Dkt John Magufuli.
Naye   Mbunge wa  Jimbo la   Mpanda   Vjijini   Moshi   Kakoso   alisema  kuwa  Jimbo lake  na   Wilaya    ya  Tanganyika  wamepata  maendeleo kwa haraka  kutokana  na  jinsi  viongozi  wanavyofanya  kazi kwa  ushirikiano  bila  kuwepo na  migogoro yoyote.
 Alisema  anamwombea heri    Mkuu wa  Wilaya  hiyo  Salehe  Mhando  asihamishwe  kwenye    Wilaya  hiyo kutokana  na  utendaji kazi wake  kwani   amekuwa akifanya kazi   mpaka  anasahau  kujenga  mwili  wake   kwa  kushindwa  hata  kula  kwa  ajiri ya majukumu  ya  kuwatumika wananchi .
Kwa upande wake mkurugenza wa  Halmashauri  hiyo  Romuli   Rojas  alisema  kuwa  Wilaya  hiyo imepiga  hatua  kubwa ya  maendeleo  kwenye  sekta  mbalimbali    kama  vile   afya ,barabara  ,mawasiliano elimu   maj, na  kilimo.


Mwisho

No comments:

Post a Comment