Tuesday 15 May 2018

kutohudhuria clinick chanzo cha vifo

Na Gurian Adolf
Sumbawanga

TABIA ya wanawake wajawazito mkoani Rukwa kuto hudhuria huduma za kliniki ni miongoni mwa sababu zinazo changia kurudisha nyuma jitihata za kukabiliana vifo vya wajawazito na watoto wachanga mkoani humo.
Mganga mkuu wa mkoa huo Bonifas Kasululu aliyasema hayo jana wakati akiwasilisha mada katika uzinduzi wa mradi wa mama na mwana mkoani Rukwa ambao utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2018 hadi mwaka 2020 na utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 25.
Alisema kuwa pamoja na elimu inayotolewa kwa wanawake mkoani humo kuhudhuria kliniki bado kumekuwa na mwitikio mdogo hali inayosababisha wanawake wengi kupoteza maisha wakati ama baada ya kujifungua kwakuwa hawapatiwi tiba ya matatizo yanayowakabili.
Kasululu alisema kuwa mwanamke mjamzito anapohudhuria klinick inakuwa ni rahisi kutibiwa magonjwa mbalimbali aliyonayo sambamba na kuangalia maendeleo ya ujauzito wake lakini inashindikana kwakuwa hawahudhurii klinick.
Alisema kuwa sababu nyingine ni tabia ya wananwake kujifungulia majumbani nayo ni changamoto kubwa kwani wapo baadhi ya wanawake wajawazito hawataki kujifungulia hospitali hali inayosababisha kupata huduma sahihi wakati wa kujifungua.
Mganga mkuu huyo wa mkoa wa Rukwa alisema kuwa tatizo linakuja pale ambapo mama mjamzito amepata changamoto ya kuvuja damu nyingi ama mtoto mchanga amepata matatizo na anahitaji huduma za kitaalamu wengiwao wamekuwa wakipoteza maisha kwa kukosa huduma hizo.

Katika uzinduzi huo mwakilishi wa wizara ya kutoka  TAMISEMI,Winan Koheleth alisema kuwa serikali bado inawatambua wakunga wa jadi na mpaka sasa hawawezi kuondolewa kutokana na uhaba wa watumishi katika wizara ya afya lakini kilichopo ni kuendelea kuwajengea uwezo.
Alisema kuwa wakunga wanapaswa kuelimishwa kuwa iwapo mama mjamzito amepata changamoto wasimng'ang'anie kumpa huduma badala yake wampeleke hospitali iliaweze kupatiwa huduma stahiki zitakazo okoa maisha ya mama na mtoto.
Akizindua mradi huo wa mama na mwana unaotekelezwa na mashirika ya Jpiego,Africare na Plan International kwa ufadhili wa serikali ya Canada mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo alisisitiza pia suala la lishe kwa watoto mkoani humo kwani unakabiliwa na kiwango kikubwa cha udumavu na utapia mlo.
Alisema kuwa takwimu zinaoshe kuwa udumavu kitaifa upo nchini kwa asilimia 32 wakati mkoa wa Rukwa upo kwa kiwango cha asilimia 56 kitu ambacho kinahitaji mikakati ya kukabiliana nao kwani ukiachwa kuendelea unasababisha madhara katika akili sambamba na kuwa kichocheo katika jitihada za kukabiliana na vifo vya akina mama wajawazito pamoja na watoto wachanga.
Mwisho

No comments:

Post a Comment