Friday 29 May 2015

Siku ya pili ya kongamano la FIFA imeaanza

Blatter anakabiliana na mpinzani wake mkuu mwanamfalme Hussein kutoka Jordan
Siku ya pili ya Kongamano la kila mwaka la FIFA imeanza huko Zurich Uswisi.
Siku ya pili ya Kongamano hilo ndio inayomchagua Rais wa FIFA.
Awali kumekuwa shinikizo kwa FIFA kuhairisha kongamano hili na pia uchaguzi wa urais.
hata hivyo maombi hayo yalifutiliwa mbali na inatarajiwa kuwa rais Sepp Blatter ataendelea mbele na uchaguzi ambao anakabiliana na mpinzani wake mkuu mwanamfalme Ali Bin al Hussein wa Jordan.
Blatter alifungua kongamano hilo kwa kuomba kuweko na umoja miongoni mwa maafisa wa FIFA.
Amesema kuwa tuhuma hizo ni njama ya kuibua maswali dhidi ya uwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa 2018 na 2022.

Blatter amesema kuwa tuhuma zinazoenea sasa ni njama dhidi ya FIFA
Blatter aliyasema hayo alipokuwa akiwahutubia wajumbe, katika siku ya pili ya mkutano mkuu wa shirikisho hilo la kandanda duniani huko Zurich Uswisi.
Blatter ameahidi kukamilisha mabadiliko yatakayoirejeshea FIFA hadhi yake.
Blatter anakabiliana na mwanamfalme Ali Bin al Hussein wa Jordan katika uchaguzi huo utakaofanyika leo.
Kwa upande wake mwanamfalme Ali Bin al Hussein wa Jordan anasema kuwa yeye pekee yake ndiye aliye na nia ya kuleta mabadiliko ya kimsingi yatakayomaliza ufisadi na ulaji rushwa ndani ya FIFA.
Takriban wenyeviti wa mashirika 209 ya kandanda kote duniani wanakura moja kila mmoja .
Mwaandishi wa habari wa BBC, anasema kuwa Bwana Blatter anategemea uungwajji mkubwa kutoka kwa wajumbe wa mataifa ya Amerika, Afrika na Asia - ambao wanasema kuwa amefanya mengi katika kuboresha mchezo wa kandanda katika mataifa maskini.
 
FBI inachunguza uwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa 2010
Naye Prince Ali anauungwaji mkubwa kutoka mataifa ya bara Ulaya.
Wajumbe hao wawili watahitaji zaidi ya robo tatu ya kura zote ili kupata ushindi wa moja kwa moja katika mkondo wa kwanza.
Hilo lisipofanyika, kutakuwa na mkondo wa pili wa upigaji kura, ambapo mshindi wa kura nyingi atatangazwa mshindi.
FIFA imekabiliwa wimbi la tuhuma za ufisadi ulaji rushwa na ubadhirifu mkubwa baada ya maafisa wake wakuu saba kukamatwa na polisi nchini Uswisi ilikujibu mashtaka nchini Marekani.
Maafisa wa kijasusi kutoka Marekani FBI wamependekeza kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa maafisa 14 wa FIFA kwa kula mlungula wa takriban dola shilingi 150 katika kipindi cha miaka 20.

No comments:

Post a Comment