Friday 29 May 2015

Serikali yatangaza kutenga bajeti zaidi kwenye tafiti za afya.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhOWUqGpUVjZ88cJrCVLA0l2mWtqPHkvmwbTcDQ4VwO8FNjDKJx7y2YOpCFstahc2glSZhITF2XC_H-p6A_rtq3d-P4sHApLMQfFuaAqQkrG76Prix51EWpfL1pCz9tVoVMPfJFUDFvOg4/s1600/PICHA+1.JPG


 Naibu wa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi, Mh. Anne Kilango  akisisitiza jambo  mbele ya  Madaktari na wanafunzi wa udaktari kutoka Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) waliohudhuria Mkutano Mkuu wa tatu wa sayansi ya afya ulioandaliwa na chuo hicho  jijini Dar es Salaam jana. Kwenye mkutano huo wa siku mbili huku ukilenga  kujadili masuala ya tafiti kwenye sayansi ya afya, Mh. Kilango alimuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Mohamed Gharib Billal.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjH_Cis3J-xeNdQ0PXGezPcN83EvJs-uPLvsmt1-bv8wWGep3cveQb5vdh7oCY5wezeRP8aQ9rB9h6rG_LRXd2P449pLZigpgiS8LEHpqAn28lyPuQk0Bhm_xu_4R-l8Lc0NY1u6JE5EZ4/s1600/PICHA+2.JPG

 Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Anna Kilango (kulia) akijadiliana jambo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof.Ephata Kaaya, mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa tatu wa sayansi ya afya ulioandaliwa na chuo hicho  jijini Dar es Salaam jana.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi4VKghpmJuFgPFpN7Nb8zqIVKlxsakS6hJN5OOaVUFQGBysfj4ZTFOqIAV80XpgbJSyFC5pj8KrfHhN_4sc0cxFiyGSJppyyDE7e44YxsCY0msqlY9zJ1Bfve7fFeaBnN0lflAOgPELj0/s1600/PICHA+3.JPG
Baadhi ya wanasayansi, Madaktari na wanafunzi wa udaktari kutoka  Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) wakifuatilia kwa umakini Mkutano Mkuu wa tatu wa sayansi ya afya ulioandaliwa na chuo hicho  jijini Dar es Salaam jana.

Naibu wa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi, Mh. Anne Kilango  amebainisha kuwa bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2015/16 imeongeza fungu zaidi kwenye masuala ya utafiti hususani ule wa sayansi ya afya.

Mh. Kilango alitoa kauli jijini Dar es Salaam jana wakati akifungua  Mkutano Mkuu wa tatu wa sayansi ya afya ulioandaliwa na Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) na kuhudhuliwa na mamia ya Madaktari na wanafunzi wa udaktari kutoka chuo hicho.

“ Ili taifa liweze kufanya vizuri kwenye sekta yoyote ile ni lazima tuwekeze zaidi kwenye masuala ya tafiti. Kwa kulitambua hilo napenda kuwataarifu kuwa hata kwenye bajeti yetu ya mwaka huu wa fedha tunatenga kiasi kikubwa cha rasilimali fedha kwa ajili ya kuwezesha tafiti hizi zikiwemo hizi za masuala ya afya,’’ alisema Mh. Kilango ambaye alimuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Mohamed Gharib Billal.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof.Ephata Kaaya alisema kuwa kwa sasa taifa linahitaji zaidi tafiti za kiafya hususani kwenye magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo kisukari, shinikizo la damu na saratani.

“ Ni dhahiri kuwa kwa sasa magonjwa haya yasiyo ya kuambukiza yamekuwa ni tishio kwa taifa. Kama wataalamu wa masuala ya afya tunaona kuja tija zaidi tukiwekeza katika tafiti zinazohusu pia magonjwa haya,’’ alibainisha.

Mkutano huo wa siku mbili unatarajiwa kuhitimishwa leo ambapo zaidi ya tafiti 100 kuhusu maswala ya afya zitawasilishwa.

No comments:

Post a Comment