Friday 29 May 2015

Issue ya Shilole yatua mjengoni


Sakata la Mwanamuziki Shilole kucheza  huku baadhi ya sehemu za matiti zikiwa wazi limechukua sura mpya Bungeni leo kufuatia Naibu Waziri wa Habari vijana na Utamaduni na Michezo Juma Nkamia kutangaza kuwa  inasubiria uamuzi wa Baraza la sanaa Taifa (Basata).
 
Aidha, Nkamia amesema   suala la shilole hivisasa lipo chini ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)  ambapo mara baada ya kumaliza mahojiano naye litapelekwa wizara ya habari vijana na utamaduni  na michezo kwa hatua nyingine zaidi.
 
Hivi karibuni Shilole  aliwaomba  msamaha watanzania  kwa madai kuwa anajutia kutozingatia maadili katika onesho hilo lililofanyika nchini Ubelgiji na  kuzua gumzo nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment