Tuesday 31 July 2018

Onyo kwa makampuni ya ujenzi barabara

Na Gurian Adolf
Katavi

WAZIRI wa  ujenzi  uchukuzi na   Mawasiliano mhandisi  Isack  Kamwelwe ameyaagiza  Makampuni  ya  ujenzi   kuhakikisha kuwa  wanamwagia  maji  kwenye   sehemu za   makazi ya  watu  pindi wanapokuwa wakitengeneza  barabara ili kuwaondolea  vumbi na kuwaepusha  na  magonjwa .
Alitoa   agizo  hilo jana kwa  nyakati   tofauti katika  maeneo ya   Majalila   Wilayani   Tanganyika  na   katika   Kijiji  cha   Inyonga  Wilayani   Mlele mkoani Katavi wakati akikagua   ujenzi wa  barabara  kwa  kiwango cha   lami  kutoka   Mpanda mkoani katavi   hadi   sikonge   Mkoani Tabora.

Alisema kuwa  kumekuwa  na  tabia ya  wakandarasi wa  makampuni ya  kichina wanaotengeneza  barabara  kwenye   maeneo  mbalimbali hapa   nchini  kutomwagilia  maji  kwenye  maeneo ya  makazi   wanayoishi   watu hivyo kuwasababishia kero kubwa ya vumbi.
  Alisema kuwa ni wajibu  wa  kila  kampuni  inayotengeneza  barabara  kumwagia  maji  kwenye maeneo  wanayoishi  watu  kwani  kwenye  mikataba  yao wanatakiwa  kufanya  hivyo  na    wanalipwa  fedha na  Serikali    hivyo  swala  la  uwagiliaji wa   maji ni  la lazima.
Waziri  huyo alisema  kuwa  matokeo ya  kutomwagia  maji  kwenye  maeneo   ya  makazi  kwanasababisha  wananchi  kupata  maradhi ya   ugonjwa  wa   vifua na mafua.
  Alisema kuwa licha ya  ujenzi  wa  barabara  ya   Mpanda    Tabora  kwa  kiwango cha  lami  pia  serikali imepanga  kutengeneza  barabara  yenye   urefu wa  kilometa   128 kwa  kiwango cha  lami kutoka   Mpanda   hadi   Karema  mwambao mwa  ziwa   Tanganyika   Mkoani  Katavi .
  Aliongeza kuwa barabara  hiyo ni  muhimu  sana   kwaajiri ya  kusafirisha  mizigo  kwenda  nchi ya Demokrasia ya  Kongo kupitia   bandari  inayojengwa  karema  kwani  lengo la   Serikali ni  kutaka  kusafirishia   mizigo    kupitia    bandari ya  karema  kwenda  kwenye  miji ya  Momba  na  Karemii  nchini  Kongo .
Pia  alisema serikali imepanga  kuanzisha   safari za  ndege  katika  uwanja wa  ndege wa   Mpanda  ifikapo  mwezi  desemba  mwaka  huu  baada ya   Wizara ya  ujenzi na  uchuzi na  mawasiliano  kuagiza  magari  sita   ya     zima    moto   ambapo moja  litapelekwa uwanja  wa  ndege wa  Mpanda na    safari  za  ndege kutoka  Dares  salaam   hadi    Mpanda   kwani  tatizo  lilikuwa  likisababisha kutokuwepo  safari za  ndege ilikuwa  ni   uwanja  wa  Mpanda  kutokuwa na  gari ya  zima  moto .
Alisema  kuanza  kwa  safari za  ndege  kutasaidia watalii  kuongezeka  katika  hifadhi ya  Katavi kwani walikuwa wanashindwa kwenda  kwa  wingi  kutokana na kutokuwepo kwa  usafiri wa  ndege.
Naye Meneja    wa  TANROADS   mkoa  wa   Katavi   muhandisi  Martin  Mwakabenda   alisema  kuwa  kumekuwepo na   changamoto  mbalimbali  kwenye  ujenzi wa  barabara ya  kutoka    Mpanda  kwenda  mkoani Tabora  yenye    urefu wa  Zaidi ya  kilometa   340  inayotarajiwa  kukamilika  baada  ya  miezi  36.
Alitaja  baadhi ya  changamoto kuwa  ni  wizi wa  mafuta  unaofanywa  na       watumishi  wasio  waaminifu wa  vibarua  wanaoshirikiana  na    wananchi  wanaoishi  jirani  na  Kambi  za   ujenzi wa  barabara .

Mmoja wa wakazi wa    Kijiji  cha   Inyonga John  Samoja alimweleza   Waziri   Kamlwelwe kuwa  wamekuwa  wakipata tabu sana kutokana na vumbi  kwenye  maeneo  wanayoishi  hivyo  wanaomba  wakandarasi  wawe  watii agizo la waziri siku zote na si  tu  kumwagia  maji  pindi  wanapo  sikia   waziri anafanya ziara ya kukagua barabara wanazo jenga.
 MWISHO

No comments:

Post a Comment