Friday 26 May 2017

Katavi yawapiga msasa waganga wa jadi

Na Walter  Mguluchuma
Katavi.

Mkoa wa Katavi una jumla ya waganga wa jadi wanaotoa tiba za asili wapatao 300 lakini kati yao ni 160 tu ndio waliosajiwa .

Hayo yamebainishwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Yahaya Hussein wakati wa mafunzo ya siku moja kwa Waganga wa Tiba asili na Tiba mbadala wa Manispaa ya Mpanda yaliofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda katika Mtaa wa Ilembo Mkoani humo.

Dkt Yahaya alisema Mkoa wa Katavi kwa kipindi cha mwaka 2012 hadi 2017 umekuwa ukitekeleza zoezi la usajiri wa Waganga wa Tiba asili na Tiba mbadala kwa kupitia ngazi ya Wilaya kwa kushirikiana na uongozi wa Waganga wa Tiba asili .

Lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha Waganga wote wanaotoa huduma hizo wanafanya kazi kwa kufuata kanuni na taratibu za Serikali na sio kinyume na matakwa ya Serikali .

Kwa Mkoa wa Katavi hadi hivi sasa kuna vituo vitatu ambavyo vinatoa huduma ya tiba mbadala.


Mkoa wa Katavi katika kuhakikisha Waganga wote wa Tiba asili na Tiba mbadala wanaofanya kazi kwa kufuata kanuni za Serikali imesha watambua zaidi ya Waganga wa Tiba asili zaidi ya 300 huku kati yao 160 wakiwa wamesajiwa .

Hayo yalisemwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Yahaya Hussein wakati wa mafunzo ya siku moja ya Waganga wa Tiba asili na Tiba mbadala wa Manispaa ya Mpanda yaliofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda katika Mtaa wa Ilembo Mkoani humo.

Dkt Yahaya alisema Mkoa wa Katavi kwa kipindi cha mwaka 2012 hadi 2017 umekua ukitekeleza zoezi la usajiri wa Waganga wa Tiba asili na Tiba mbadala kwa kupitia ngazi ya Wilaya kwa kushirikiana na uongozi wa Waganga wa Tiba asili.

Lengo ikiwa ni kuhakikisha Waganga wote wanaotoa huduma hizo wanafanya kazi kwa kufuata kanuni na taratibu za Serikali na sio kinyume na matakwa ya Serikali.

Kwa Mkoa wa Katavi hadi hivi sasa kuna vituo vitatu ambavyo vinatoa huduma ya tiba mbadala ambavyo alivitaja kuwa ni Sigwa herbalist,Huruma herbalist na Sanitarium herbalist.

Dkt Yahaya alifafanua kuwa Mkoa wa Katavi unajumla ya waganga wa Tiba asili na Tiba mbadala 316 na hadi sasa Mkoa umefanikisha usajiri wa Waganga wa Tiba Asili na Tiba mbadala 165 na bado uhamasishaji unaendelea kwa kushirikiana na waratibu wa Wilaya .




 Washiriki wa  mafunzo ya  waganga wa Tiba  asili na  tiba  mbadala wa Wanispaa ya Mpanda
Nae Mkurugenzi msaidizi kutoka Wizara ya Afya Dkt Paul Mhume alisema wamepanga kutoa mafunzo hayo kwa waganga wa Tiba asili na Tiba mbadala katika Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi .

Lengo la mafunzo hayo ni kuwahamasisha Waganga wa Tiba asili na Tiba mbadala ili wazingatie maelekezo ya Serikali ya kufanya kazi baada ya kuwa wamesajiliwa kwanza.

Msajiri wa Baraza la Tiba asili na Tiba mbadala Dkt Ruth Suza alisema huduma za tiba asili zinatambuliwa rasmi kwa mujibu wa sera ya afya na sheria ya tiba asili na tiba mbadala Namba 23 ya mwaka 2002 na madhumuni ya sheria hiyo ni kusimamia,kudhibiti na kuendeleza tiba asili ya Tanzania .

Alisema Baraza la Waganga wa Tiba asili na Tiba mbadala limeundwa kama chombo kikuu cha Serikali kinasimamia na kuratibu shughuli hizo.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Kamishna wa Polisi Paul Chagonja aliwataka waganga hao wazingatie sheria na kanuni zinazohusu huduma za tiba asili na pia waache kujihusisha na ramli chonganishi.

Alisisitiza kuwa kila mtoa huduma wa tiba za asili awe na utaratibu wa kuwarufaa wagonjwa katika vituo vya tiba za kisasa kwa lengo la kupunguza vifo hususani vya akina mama wajawazito na watoto.

Mwisho




No comments:

Post a Comment