Tuesday 31 July 2018

Elimu ya hitajika kwa wanafunzi waachane na dada poa

Na Gurian Adolf
Katavi
BARAZA la madiwani la  Manispaa  ya Mpanda mkoani Katavi  limeshauri  itolewe elimu  kwa wanafunzi wa  shule  za   Sekondari  na  Msingi katika manispaa hiyo ili  wajiepushe na tabia ya kunua wakina dada wanaouza miili ya maarufu kama dada poa ili kuwakinga na magonjwa mbalimbali ya ngono.
Ushauri huo ulitolewa jana kwenye  kikao  cha baraza la madiwani la  manispaa  hiyo  kilichofanyika  katika   ukumbi wa  mikutano wa  manispaa  ya Mpanda  kilichoongozwa  na  Meya  wa Manispaa hiyo Willy   Mbogo.
 Awali  katika  kikao  hicho   Mwenyekiti wa  kamati ya  kudhibiti  ukimwi  Lucas  Kanoni wakati akiwasilisha  taarifa  ya  kamati  hiyo  alisema  kuwa  biashara ya akina  dada ya kuuza  miili yao  imekuwa ni tishio kubwa hivi sasa katika Manispaa hiyo .
Alisema  kuwa  madada  poa  hao   kwasasa  wameanza    kufanya   biashara ya  kuuza  mili yao  kwa  kujishusha  na  kuanza  kufanya  ngono  na  wanafunzi wa  shule hadi za  msingi  jambo   ambalo ni  hatari kwa   watoto hao kutokana na kuwepo kwa magonjwa ya ngono kama ukimwi.
Kanoni  alisema kuwa  yapo maeneo  mbalimbali  katika Manispaa  hiyo   ambayo yamekuwa ni  maarufu  kwa  biashara  hiyo ambayo    aliyataja  kuwa ni  mtaa wa   Fisi  ulioko     katika  Kata  ya   Majengo  B  ,M taa  wa   Simba  ulioko  Kata  ya   Majengo  B, Kakese  na  Mwamkulu .
Naye diwani wa  Kata  ya   Kashaulili  John  Matongo aliliambia   baraza  hilo la  madiwani kuwa  hivi sasa  elimu  ni  muhimu ikatolewa  kuanzia  shule za msingi  ili kuwaelimisha  wanafunzi  waweze kuacha kuwa wateja wao na pia kujikinga magonjwa ya ngono.
 Alisema   endapo    hatua  za  haraka   hazitachukuliwa   kutokana  na  kushamilikwa  biashara hiyo upo   uwezekano   mkubwa  wa kuongezeka  kwa mitaa  mingine  ambayo haina  sifa ya   biashara  hiyo  ya  dada  poa  kama  ilivyo kwa mitaa ya   simba  na  fisi .
 Kwaupande wake meya  wa  Manispaa  ya   Mpanda   Wily Mbogo    alisema  kuwa ni  vema watoto  waanze kufundishwa  toka  wakati wakiwa wadogo wakiwa mashuleni  kutojihusisha  na  kufanya  mambo   ambayo hayalingani na  umri wao kama  vile kufanya  ngono.
 Alifafanua kuwa  endapo kama  hawatapewa elimu  mapema ya  kujiepusha  na  kufanya  ngano wakiwa  na   umri  mdogo  upo   uwezekano wa kupata  maambukizi ya  vvu.
Katika kikao hicho mkuu wa   Wilaya  ya   Mpanda  Lilian  Matinga  alisema kuwa kwa sasa   Mkoa  wa  Katavi    ni  miongoni  mwa   mikoa  yenye  maambukizo ya   vvu  kwa kiwango cha  juu ya  wastani  wa Kitaifa .
 Alisema  maambukizi  ya   vvu  kwa  mkoa  wa   Katavi   ni  asilimia 5.9   wakati wastani wa  kitaifa  ni  asilimia  5.9  hivyo  mkoa huo  uko   juu ya  wastani  wa maambukizi ya Kitaifa.
Aliongeza kuwa  kwa  kipindi cha  miaka  mitatu  sasa  wastani  huo  wa   maambukizi  umekuwa   upo  pale  pale  bila kushuka jambo  ambalo   ni  hatari kwa wananchi  endapo  hawata   badili   tabia.
Ndiyo  maana  serikali   imepanga  kufanya  utafiti  kwenye  mikoa mitano yenye  maambukizi  makubwa  ya   maambukizi ya   vvu  ambayo ni  Songwe,  Katavi   Njombe ,Mbeya  na  Kigoma.
Mwisho

No comments:

Post a Comment