Na Gurian Adolf
Sumbawanga
JUMLA
ya watoto wa wavuvi wapatao 400 waliopo katika kambi ya wavuvi ya
Nankanga wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa ambao wamefikia umri wa kuanza
darasa la kwanza wameshindwa kupata haki yao ya elimu kutokana na
kutokuwa shule.
Diwani wa kata ya Nankanga wilayani
Sumbawanga mkoani Rukwa, Anyisile Kayuni alimwambia hayo mkuu wa mkoa
huo Joachim Wangabo wakati akiwa katika ziara ya kukagua makambi ya
wavuvi katika suala la kukabiliana na ugonjwa wa kipindu pindu.
No comments:
Post a Comment