Na Gurian Adolf,
Nkasi
KATIKA kukabiliana na tatizo la mimba kwa wanafunzi
wanaume wilayani Nkasi wameonywa kuacha mara moja tabia ya kuwaita
watoto hao wa kike
majina ya mahaba kwani yanawapelekea kujiona wamekua na kuanza kushiriki
vitendo vya ngono
Wito huo umetolewa jana na afisa elimu Sekondari wilayani
Nkasi Abel Ntupwa kwenye kikao kazi
kilichowajumuisha Wakuu wa shule 23 za sekondari wilayani Nkasi kilichomshirikisha na afisa elimu wa mkoa
Nestory Mloka kilicholenga kupeana mikakati namna ya kuboresha taaluma baada ya
wilaya Nkasi kuporomoka sana kwenye mitihani ya kitaifa.
Alisema hivi sasa watu wazima wamekua na tabia ya kuwaita watoto
hao wa kike ambao ni Wanafunzi majina ya kimahaba kama Baby kama mzaha na mwisho wa siku
ujikuta Watoto hao wanajiingiza kwenye mtego huo mbaya na hivyo kuanza kushiriki vitendo vya mapenzi.
Hivyo kufuatia hari
hiyo amedai kuwa ni marufuku kwa mtu yeyote
kumwita mtoto wa kike ambaye ni Mwanafunzi majina hayo ya Baby ili
kuwaweka Watoto hao katika hari ya usalama.
Lakini pia alikemea tabia ya baadhi ya Walimu wenye tabia ya
kujihusisha kimapenzi na Wanafunzi au hata kuwatamani kuwa hakuna dhambi kubwa
kwa Mwalimu kama hiyo na kuwa hakuna atakaebaki salama kwa kujihusisha na tabia
hizo pindi itakapobainika.
Lakini pia aliwataka Wakuu wa shule kuhakikisha kuwa wao
ndiyo wakaguzi wa kwanza katika shule zao kwa kuhakikisha kuwa Walimu wao wanafundisha
sawasawa na kuleta tija ya kitaaluma katika masomo wanayoyafundisha.
Alisema shule yoyote inayofanya vizuri ni matokeo ya uongozi
bora wa shule ambapo Walimu wakuu wameamua kuzisimamia shule zao na kuwa sasa
wameamua kuboresha elimu wilayani Nkasi nas kutaka Wakuu wa shule kusiomama
imara na kama kuna ambaye atakwenda kinyume na kasi hiyo watamshughulikia mara moja.
Kwa upande wake afisa elimu wa mkoa wa Rukwa Nestory Mloka alisema
kuwa yeyebinafsi kamwe hawezi kusita kuwavua madaraka Walimu wakuu ambao wataonyesha kushindwa
kuzisimamia shule zao ili zitoe matokeo chanya na kuwa haoni sababu kwa
wilaya Nkasi iliyokuwa inaongoza katika mkoa Rukwa sasa imeanza kushika mkia.
Alisema kwa kuanza wameanza na mabadiliko madogo ambapo
wameteua baadhi ya waratibu wa elimu kata kutoka katika shule za
Sekondari na msingi na kuwataka washirikiane nao vizuri na kuwa wanataka kuona
mwaka huu mabadiliko yanatokea lakini kinyume cha hapo alisema kuwa hatamuelewa mtu.
Mwisho
No comments:
Post a Comment