Na Gurian Adolf
Nkasi
MAHAKAMA ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa imemuhukumu Paschal Kabagi (18) kuchapwa viboko sita baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17 anzyesoma Kidato cha Kwanza katika shule ya Sekondari Nkomolo wilayani humo.
Akisoma hukumu hiyo mwishoni mwa wiki jana,hakimu wa mahakama hiyo,Ramadhani Rugemalira alisema kuwa kwa kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo akiwa na umri wa miaka 17 ataadhibiwa kwa kucharazwa viboko sita ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama yake.
Awali mwendesha mashtaka mkaguzi wa Polisi , Hamimu Gwelo alidai mahakamni hapo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Januari 12 , 2016 majira ya saa mbili asubuhi katika kitongoji cha Uwanja wa Ndege kilichopo mjini Namanyere wilayani Nkasi.
AlidaI mahakamani hapo kuwa wakati akitenda kosa hilo mshitakiwa alikuwa akisoma Kidato cha Tatu katika Shule ya Sekondari Nkasi.
Aliendelea
kuieleza mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa huyo alimvizia mwanafunzi huyo wa
kike kwenye mahindi wakati akienda shule ndipo alipo mshika kwa nguvu
na kisha kumuangusha chini na kumbaka. MAHAKAMA ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa imemuhukumu Paschal Kabagi (18) kuchapwa viboko sita baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17 anzyesoma Kidato cha Kwanza katika shule ya Sekondari Nkomolo wilayani humo.
Akisoma hukumu hiyo mwishoni mwa wiki jana,hakimu wa mahakama hiyo,Ramadhani Rugemalira alisema kuwa kwa kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo akiwa na umri wa miaka 17 ataadhibiwa kwa kucharazwa viboko sita ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama yake.
Awali mwendesha mashtaka mkaguzi wa Polisi , Hamimu Gwelo alidai mahakamni hapo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Januari 12 , 2016 majira ya saa mbili asubuhi katika kitongoji cha Uwanja wa Ndege kilichopo mjini Namanyere wilayani Nkasi.
AlidaI mahakamani hapo kuwa wakati akitenda kosa hilo mshitakiwa alikuwa akisoma Kidato cha Tatu katika Shule ya Sekondari Nkasi.
Mshtakiwa alijitetea kwa kuiomba mahakama imsamehe kwa kuwa hakujua kuwa alichokifanya kilikuwa kosa kisheria utetezi uliopingwa na mwendesha masthaka na kisha mahakama hiyo ikaamua kutoa hukumu hiyo .
Mwisho
No comments:
Post a Comment