Na Gurian Adolf
Sumbawanga
MKUU
wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo ameiagiza halmashauri ya wilaya ya
Sumbawanga mkoani humo kutafuta fedha ili ijenge mwalo wa Nankanga
katika ziwa Rukwa utakao wasaidia wavuvi kufanya biashara ya samaki na
utakuwa ni chanzo kizuri cha mapato kwa halmashauri hiyo.
Agizo
hilo alilitoa jana wakati alipokuwa akifanya ziara ya kukagua makambi
ya wavuvi wa samaki katika jitihada za kukabiliana na ugonjwa wa
kipindupindu uliotokea wilayani humo tangu mwezi Novemba mwaka jana
ambapo usababisha vifo vya watu nane na 270 kuugua ugonjwa huo.
Alisema
kuwa ufukwe uliopo katika makambi ya wavuvi ya Nankanga katika ziwa
Rukwa wilayani Sumbawanga linafaa kwaajili ya kujenga mwalo ambapo
wavuvi watakuwa wanafanya biashara ya samaki na kisha halmashauri kupata
fedha kwa kutoza ushuru.
''naagiza halmashauri ya wilaya
ya Nkasi itafute fedha ili ijenge mwalo huu wa Nankanga kwani eneo hili
ni zuri kwa wafanyabiashara kuuzia samaki ambapo pia itakuwa ni chanzo
kizuri cha mapato kwakuwa mtakusanya ushuru na halmashauri yenu itapata
fedha''
Alisema kuwa wilaya hiyo imejaliwa fursa nyingi
ambazo kama zikitumika ipasavyo zitaongeza makusanyo na halmashauri
itapata fedha nyingi na itaweza kuwahudumia wananchi ili waaweze
kuondokana na changamoto mbalimbali zinazo wakabili.
Alisema
kuwa nilazima itafutwe namna fedha zipatikane haraka na mwalo huo
ujengwe kwakuwa wananchi wanahitaji huduma nzuri kwani ni jukumu la
watendaji kuzitambua fursa zilizopo na kuzitumia ipasavyo.
Awali
akitoa taarifa ya ugonjwa wa kipindupindu katika halmashauri hiyo Kaimu
mkurugenzi ambaye ni Mganga mkuu wa wilaya hiyo Fani Musa alisema kuwa
kipindupindu kimedhibitiwa licha ya kuwa bado jitihada zinahitajika
kutoa elimu ya afya kwa wavuvi.
Alisema kuwa changamoto
iliyopo ni kutotumia maji safi na salama kwani baadhi ya wavuvi
wanakataa kutumia maji yanayotibiwa kwa dawa aina ya waterguard kwamadai
kuwa hayana radha.
Mwisho
No comments:
Post a Comment