Gurian Adolf
Sumbawanga
BAADHI
ya wazazi katika mji wa Matai wilayani Kalambo mkoani
Rukwa wamelalamikia kitendo cha mtendaji wa kijiji
hicho Ester Mwashambwa kuwakamata watoto wao ambao ni wanafunzi wa
shule ya msingi Matai A na kisha kuwafungia katika ofisi yake kwa zaidi
ya masaa 10 bila kula wala kunywa kwa madai kuwa anafanya hivyo ili
wazazi wao wafike kulipa faini kwa kosa la watoto hao kuto kwenda
shuleni.
Akizungumza
na rukwakwanza.blogspot.com i kwa niaba ya wazazi wengine mmoja wa wazazi hao Mulele
Mulenga alisema kuwa tukio hilo lilitokea jana ambapo afisa mtendaji
huyo akishirikiana na mwenyekiti wa kijiji Nikasi Kamande waliwakamata
watoto wao na kisha kuwafungia katika ofisi ya kijiji kwa madai kuwa
hawaendi shuleni na iwapo mzazi alifika kumkomboa mtoto wake alipaswa
alipe faini ya shilingi 10,000 ili aachiwe mtoto wake.
Alisema
kuwa mtendaji wa kijiji wakishirikiana na mwenyekiti wa kijiji pamoja
na mgambo wa kijiji hicho waliendesha operesheni ya kuwakamata wanafunzi
ambao walikuwa na sare za shule lakini waliwakuta mitaani na kisha
kuwafungia katika ofisi ya kijiji kwa madai kuwa hawajaenda shule na
shule yao ilikuwa imefunguliwa siku hiyo ya jumatatu baada ya likizo ya
mapumziko ya pasaka.
Mulenga ambaye alikuwa akizungumza kwanjia ya simu na mwandishi wa rukwakwanza.blogspot.com alisema kuwa siku ya tukio hilo yeye alimuacha nyumbani mtoto aitwaye Tumain Mlele(9) ambaye ni mtoto wa kaka yake akiwa anajiandaa kwaajili ya kwenda shule kisha yeye akaenda shambani.
Alisema
kuwa aliporudi jioni kutoka shambani aliambiwa kuwa Tumaini amekatwa
pamoja na wanafunzi wengine na wamefungiwa katika ofisi ya mtendaji kwa
kosa la kuto kwenda shule ambapo alikwenda katika ofisi hiyo ya kijiji
na alifika ilikuwa majira ya saa 2;08 za usiku ambapo alimkuta mtoto
huyo akiwa na wanafunzi wengine wanne ambao walikuwa hawajakombolewa na
aliwakuta wazazi wao wakibembeleza kupunguziwa faini ili walipe
wawachukue watoto wao.
Mulenga
alisema kuwa baada ya kumuona mtoto wake huyo alijisikia uchungu sana
kwakuwa alikuwa hajala chakula kutwa nzima huku watoto hao wakiwa
wamejisaidia katika ofisi hiyo ya mtendaji ambapo alichukia na kuanza
kumfokea mtendaji huyo hali ambayo iliibua zogo baina yao.
‘’Ndugu
mwandishi kwakweli roho iliniuma sana baada ya kuona watoto wetu wakiwa
wamefungiwa katika ofisi ya mtendaji wa kijiji na wakiwa wamejisaidia
haja ndogo humo humo kama nguruwe wako zizini nilitamani nirushe ngumi
lakini nikaona ntakua nimevunja sheria’’…alisema Mulenga
Baada
ya mwandishi kumsikiliza mzazi huyo alimtafuta Afisa mtendaji
mwashambwa kwa njia ya simu alikata simu na alipo muandikia ujumbe
mfupi na kujitambulisha na kutaka ufafanuzi kuhusiana na malalamiko
hayo ujumbe huo ujumbe ulimfikia lakini haukujibiwa na baada hapo simu
hiyo ikazimwa na hakupatikana tena.
Hata
hivyo mwandishi wa habari hii alimtafuta afisa mtendaji wa kata ya
Matai B, Mozes Nkinda ili aweze kujua pengine mwenyekiti wa kijiji hicho
alikuwa akitekeleza sheria walizojiwekea katika kata yao kupitia kikao
cha maendeleo ya kata WODC simu yake iliitwa lakini ikakatwa na
alipomwandikia ujumbe naye simu yake haikuweza kupatikana tena.
Kutokana
na hali hiyo ndipo alipotafuta mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya
Nkasi Simoni Ngagani na baada ya kumpigia simu ilikatwa ndipo alipo
mwandikia ujumbe huu
".Mkurugenzi habari za kazi! Pole na majukumu.
Samahani Mimi ni mwandishi wa habari naitwa Gurian Adolf nimekupigia
simu naona haijapokelewa. Samahani nia yangu ni kutaka ufafanuzi kutoka
kwako maana Jana nilipokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa kijiji
cha Matai walalamikia kitendo cha Mtendaji wa kijiji cha Matai (B) Ester
Mwashambwa kuwafungia watoto wao ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi
Matai B, akishirikiana na Mwenyekiti wa kijiji hicho Nikasi Kamande
waliwafungia ofisini kwake kutwa nzima bila kula chakula kwamadai kuwa
anawashikilia kwa kosa la kutokwenda shule ili wazazi wao wafike walipe
faini ya sh 10,000 ndipo awaachie'' hakujibu kitu.
Nimempigia simu Mtendaji huyo
hakupokea, nikamuandikia ujumbe mfupi kutaka kujua alikua anatekeleza
hilo kupitia sheria gani, meseji ilipoingia amezima na simu. Sasa
nimeona niwasiliane na wewe mwenye Halmashauri huenda nikapata
ufafanuzi zaidi. Ni hilo tu. Kazi njema". hakujibu kile mwandishi wa
habari alichomwandikia.
Hata
huyo alizungumza na katibu Tawala wa Wilaya hiyo Frank Sichalwe
alikiri kupata taarifa za tukio hilo lakini alisema kuwa bado anasubiri
taarifa kamili kutoka kwa watendaji wa halmashauri hiyo ili aweze
kufahamu kwa undani nini hasa kilitokea na hatua gani ziweze
kuchukuliwa kufuatia tukio hilo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment