Tuesday 25 April 2017

Mwenyekiti wa CCM awawa kwa kucharangwa mapanga

Walter  Mguluchuma 
Katavi.

Mwenyekiti wa  CCM  wa Tawi  la  Itenka  Kata ya  Itenka  B  Tarafa  ya  Nsimbo  Wilayani  Mpanda   Mkoani  Katavi  Hapiam   Salvatory(50)  ameuwawai kwa kukatwa kaatwa na  mapanga  katika  sehemu  mbalimbali za  mwili wake  na  kichwa kutenganishwa na  kiwili wili cha mwili wake.

Kwa  mujibu wa  Kamanda wa  Jeshi  la  Polisi wa  Mkoa wa  Katavi  Damas  Nyanda   aliwaeleza  wandishi wa  Habari  kuwa tukio  hilo la mauaji lilitokea April 24  majira ya saa  saba  mchana.

Alisema  kuwa  siku  hiyo ya tukio Hapiam aliaga nyumbani  kwake kuwa   anakwenda  mtoni  kwenye   shughuli  zake  alizokuwa  akifanya kila  siku  za kuvua samaki  kwenye mto Itenka  uliopo   Kijijini hapo.

Wakati  akiwa njiani kuelekea  mtoni  alivamiwa na watu  ambao walikuwa na  mapanga  na kumkatakata   katika  sehemu mbalimbali za  mwili wake  na kuutenganisha  kiwili wili  na  kichwa   hadi kufariki  Dunia hapo hapo.

Kamanda Nyanda  alieleza  kuwa  baada ya   wauaji  hao  kufanya  mauwaji ya kikatili na yakusikitisha  waliondoka na kutokomea kusiko  julikana  na kuuacha  mwili wa  Mwenyekiti huyo ukiwa  barabarani.

Wananchi  wawili  ambao wakuwa wakipita  kwenye  eneo  hilo waliuona mwili huo  ndipo walipokwenda kutoa taarifa kwa  uongozi wa  Kijiji  ambao nao walitoa  taarifa  kwa  jeshi la  Polisi,  ambalo lilifika  kwenye  eneo hilo  huku wakiongozwa na  yeye   Kamanda wa Polisi wa Mkoa  wa  Katavi  na   walikuta mwili wa  marehemu  huyo ukiwa umelazwa  barabarani..

Kamanda   Nyanda  alisema  kabla ya tukio  hilo   marehemu  aliwahi kuandikiwa  barua   mbili miaka   miwili  iliyopita ya kutishiwa kuuwa na watu wasio  julikana walikuwa wakimtuhumu kuwa ni  mchawi.

Alieleza  kuwa  katika  tukio  hilo  watu  watatu  wanashikiliwa na  jeshi la  Polisi kwa tuhuma za  mauaji  hayo.

Kamanda   Nyanda   ametoa  wito kwa  wananchi wa   Mkoa  wa  Katavi  kuacha  tabia ya kujichukulia  sheria  mikononi  kwani kufanya  hivyo ni  kosa kisheria.
mwisho

No comments:

Post a Comment