Wednesday 26 April 2017

Watanzania wautakia kheri na fanaka Muungano

Gurian  Adolf
Sumbawanga
Waziri wa Nchi anayeshughulia masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba, amesema kuwa changamoto za Muungano wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar zimetatuliwa kwa kiasi kikubwa kutoka 15 mwaka 2006 hadi kufikia changamoto 3 kwaka huu 2017, Muungano umetimiza miaka 53.

Waziri Makamba amezungumza hayo leo Mjini Dodoma alipokuwa katika mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na waratibu wa sherehe za kitaifa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na Walemavu na kusimamiwa na Waziri Mwenye dhamana Mhe Jenista Mhagama.
   Picha hii ilipigwa tarehe na mwezi kama wa leo 26/4  miaka 53 ilyopita ambapo hayati baba wa taifa Mwl Julisu K. Nyerere alipokuwa akichanganya mchanga kutoka nchi ya Tanganyika na nchi ya Zanzibar kisha ikazaliwa nchi ya Tanzania.

Mhe. Makamba amezitaja changamoto zilizobakia kuwa ni pamoja na usajili wa vyombo vya moto unaorahisisha kusafirisha magari kutoka Zanzibar kwenda Bara na kutoka Bara kwenda Zanzibar na kusema kuwa swala hili linafanyiwa kazi kwa kumalizwa kwa taratibu za kisheria.

Alisema kuwa changamoto nyingine inahusu Hisa za Zanzibar kwa iliyokuwa bodi ya safari ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Pamoja na Mapendekezo ya tume ya Pamoja ya fedha.

Awali akizungumzia Muungano huo unaotimiza miaka 53, Waziri Makamba Alisema kuwa umekuwepo kisheria na umerasimisha udugu na ushirikiano uliyokuwepo kati ya Bara na Visiwani.

 Hiyo hapo juu ndiyo kauli mbiu ya maadhimisho ya muungano kwa mwaka huu ambapo maadhimisho hayo yataongozwa na amiri jeshi mkuu wa vikosi vya ulinzi na usalama wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli na sherehe hizo zinaadhimishwa kitaifa mkoani Dodoma.

rukwakwanza.blogspot.com inautakia kheri fanaka na maisha marefu muungano wa zikizokuwa nchi hizi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar na kuzaliwa kwa Tanzania miaka 53 ikiyopita.

Hakika  ni muda mrefu ambao hata mataifa mengi makubwa na tajiri,yenye nguvu za kiuchumi na kijeshi yameshindwa lakini sisi tunaweza.

Tuendelee kuwa pamoja na viongozi wetu waendelee kuuenzi, tuwapuuze watu wachache wasioutaka muungano wetu inawezekana kwa maslahi yao wenyewe na si  ya wanamuungano huu. 

kwani hivi sasa dunia inafikiria katika kuungana ndipo  nguvu inakuwa kubwa kwa kila jambo.

Mfano hata  wafanyabiashara wakubwa na wadogo wanashauriwa kuungana kwa kitendo hicho huwawezesha kuwa na nguvu zaidi ya kimtaji na kuweza kufanya makubwa zaidi.

Lakini hata  maneno na methali zetu zimekuwa zikituasa "umoja ni nguvu" popote palipo umoja inamaana kuna muungano.

Katika kila muungano changamoto huwa hazikosekani, na iwapo walioungana wakikosa changamoto basi ujue yupo ambaye anavumilia tu ama  amekubali kuumia ili amfurahishe mmoja kati ya hao wawili.

Nitashangaa sana kama changamoto zitamalizika kwa kuwa zinaweza tatuliwa zilizopo lakini mbele ya safari zikaibuka nyingine kutokana na wakati, mazingira, maslahi na kizazi.

Kubwa zaidi ni sisi watanzania kutafuta namna  bora ya kuzitatua changamoto husika kila zinapotokea, kuliko kufikiria kutengana.

Hakika  hili  ni tunu ambalo  waasisi wetu wametuachia na hatunabudi kuuenzi lakini tukitatua changamoto zinazoibuka.

rukwakwanza.blogspot.com inautakia maisha marefu muungano wetu Leo na kwa vizazi vijavyo kwani bado faida za kuungana ni kubwa kuliko kutengana.

                                       Kila lakheri muungano wetu.

No comments:

Post a Comment