Sumbawanga
WAUZAJI
wa pembejeo za kilimo mkoani Rukwa wameonywa kuacha kufanya mzaha wa
kuuza pembejeo bandia kwani athari zake ni kubwa na zinaathiri uchumi wa
mkulima mmoja mmoja mpaka taifa kwa ujumla.
Onyo
hilo limetolewa na Mkuu wa mkoa huo Zelote Steven wakati
akifungua mafunzo ya siku tatu kwa wauza pembejeo za kilimo katika mkoa
huo yaliyo fadhiliwa na shirika la maendeleo la Uholanzi SNV ambayo
yanalengo la kuwajengea uwezo ili waweze kuuza pembejeo ambazo ni
sahahi ili kuepusha hasara kwa wakulima.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Zelote Steven akihutubia wauza pembejeo za kilimo wanao hudhuria mafunzo ya siku tatu katika ukumbi wa mikutano uliopo katika ukumbi wa jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa
Alisema
kuwa hivi sasa si wakati kwa wafanyabiashara ya pembejeo kufanya mzaha
katika biashara hiyo kwani kitendo cha kuuza pembejeo bandia kimekua
kikisababisha hasara kwa wakulima na hivyo inabidi kikemewe kwa nguvu
zote.
Mkuu huyo wa mkoa
alisema kuwa imefika wakati suala hilo lazima limalizwe kabisa mkoani
Rukwa kwani mkoa huo umekuwa ukitegemewa kuzalisha chakula kwaajili ya
taifa na iwapo suala hilo likifumbiwa macho ni kulitia hasara taifa.
Aliziagiza
mamlaka zinazohusika katika kudhibiti ubora wa pembejeo hizo katika
mkoa wa Rukwa kuhakikisha zinawajibika ili kuondoa pembejeo hizo kwani
wafanyabiashara hao wakiachwa wafanye wanavyotaka watasababisha hasara
kubwa.
Wauza pembejeo za kilimo kutoka katika wilaya zote za mkoa wa Rukwa wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Rukwa Zelole Steven wakati akifungua mafunzo ya siku tatu yenye lengo la kuwajengea uwezo ili waepuke kuuza pembejeo za kilimo za bandia mkoani humo.
Hata hivyo
alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inatilia mkazo katika suala la
viwanda hivyo kama uzalishaji wa mazao utaathiriwa na wauza pembejeo
kwa kuwauzia wakulima pembejeo bandia viwanda hivyo havitapata
malighafi za kuzalisha bidhaa hivyo suala la kuongeza thamani
litashindikana kwakua wakulima hawatazalisha kwa tija.
Akitoa
taarifa ya utekelezaji wa mradi miradi ya shirika hilo, meneja mradi wa
SNV Robert Kessy alisema kuwa shirika hilo lilianza shughuli zake
katika mkoa huo tangu mwaka 2015.
Alisema
kuwa shirika hilo linajikita katika Miradi ya kilimo, Maji na nishati
ambapo linawajengea uwezo wananchi ili waweze kufanya vizuri katika
uzalishaji katika sekta ya kilimo, kuhifadhi Maji na kutunza nishati ili
iweze kuwe endelevu.
Mwisho
No comments:
Post a Comment