Gurian Adolf
Sumbawanga
KATIBU
tawala wa mkoa wa Rukwa Tikson Nzunda amewalaumu baadhi ya wahubiri wa
Injili mkoani humo ambao wanahubiri huku wakiwaacha waumini wao
wakiamini kuwa wanauwezo wa kuponya ukimwi kwa maombezi.
Katibu
tawala huyo aliwalaumu wahubiri hao wa neno la Mungu kwa
kupitia barua yake aliyoviandikia vyombo vya habari vilivyopo mkoani
humo kuwaambia wahubiri hao waache kuhubiri habari hizo kwani
zinapingana na jitihada za kukabiliana na ugonjwa huo na ni upotoshaji
mkubwa.
Aliye katikati na amevaa miwani ndiye Tixson Nzunda katibu tawala mkoa wa Rukwa
Katika barua yake
Nzunda aliviandikia vyombo vya habari kuwaeleza wahubiri hao kutafuta
namna nyingine ya kuhubiri lakini kwa kutumia baadhi ya watu
wanaowaombea kushuhudia kuwa wamepona virus vya ukimwi kunasababisha
baadhi yao ambao walikuwa wanatumia dawa za ARV za kufubaza virusi
hivyo kuacha kutumia wakiamini kuwa wamepona.
Alieleza
kuwa kitendo hicho kinakinzana na jitihada za serikali katika
kuwahudumia watu wanaotumia dawa za ARV kwani baadhi yao huamua kuacha
kutumia dawa hizo wakiamini kuwa wamepona kupitia maombi ya wahubiri hao
wa injili.
Katibu
tawala Nzunda aliwataka kuhubiri neno la Mungu kuacha upotoshaji huo
wanauwezo wa kuombea watu wakapona virusi vya ukimwi kwani kitendo hicho
kinapelekea watu wanaotumia dawa hizo kuacha kutumia.
Kutokana
na mahubiri pamoja na maombezi hayo baadhi ya watu wamekuwa
wakijitokeza kwa wingi kwaajili ya kuombewa shida na magonjwa mbalimbali
ikiwemo virusi vya ukimwi.
Hata
hivyo hivi sasa mkoani humo kumekuwa na wahubiri wakiombea watu Wenye
shida na magonjwa na kisha kutumia redio zilizopo mkoani humo kuhubiri
na kuwahoji ili washuhudie kuwa wamepona magonjwa mbalimbali ikiwemo
virusi vya ukimwi.
Mwisho
No comments:
Post a Comment