Sunday 23 April 2017

Walimu wakesha kwa kuogopa kubomokewa na nyumba

Walter Mguluchuma
Katavi

WALIMU wa shule ya Msingi  Mtapemba  katika  Halmashauri ya  Nsimbo  Wilaya ya   Mpanda  Mkoani  Katavi wanalazimika kukesha pindi mvua zinapoanza kunyesha nyakati za usiku kutokana na kuvuja na hofu ya kubomokewa na nyumba za shule ambazo zimechakaa kiasi cha kutofaa kuishi binadamu.

 Nyumba ya Mwalimu Mkuu  wa shule hiyo pia haina  hata choo hali inayomsababishia usumbufu yeye na familia yake wakati wa usiku pindi wanapotaka kujisaidia kwani wakati wa mchana wamekuwa akienda kuomba kujisaidia katika vyoo vya majirani zake.

Shule  hiyo ya  Msingi  ambayo  ilijengwa  zaidi ya  40 iliyopita  ipo  umbali wa kilometa  kumi na tano  kutoka  Manispaa ya  Mji wa  Mpanda  inajumla ya walimu 16.

                         Mfano wa nyumba mbovu zilizojengwa kwa tope

Walimu wa  shule  hiyo wanalazimika kuishi kwenye  nyumba za  kupanga  kijijini  hapo  na   wengine kuishi  katika kijiji cha jirani kutokana  na  shule  hiyo kuwa na  uhaba wa  nyumba za  walimu.

Nyumba  ambayo imejengwa kwa ajiri ya  kuishi  mwalimu Mkuu   wa  shule  hiyo  haina choo  hali  ambayo  inafanya  mwalimu  anae ishi kwenye nyumba  hiyo  kutumia   vyoo vya kuomba kwa jirani zake hali ambayo inamvunjia heshima na inamfanya ajisikie aibu kuomba kujisaidia kwa majirani yeye pamoja na familia yake.

 Baadhi ya  nyumba  zilizopo   katika  shule  hiyo  ni  chakavu sana  na  hazifai  kuishi na zimejengwa kwa tofali udogo sio  tofali za kuchoma na hivyo si nyumba imara na zinaweza kubomoka wakati wowote.

Mmoja wa walimu  anae  ishi kwenye  nyumba  hizo  ambae  hakutaka kutaja jina  lake  alisema  huwa wanalazimika kutolala usiku pindi mvua zinapokuwa zinanyesha kutoka  na nyumba wanazoishi kuvuja na hofu ya kuangukiwa na nyumba hizo ambazo si imara kutokana na kujengwa kwa matofali ya tope.

Kwa upande wake Diwani wa Kata  hiyo ya Mtapemba Elieza Fyula  alikiri kuwaepo kwa  tatizo la  uhaba wa  nyumba  katika  shule  hiyo kwa kipindi  kirefu  sasa na alisema kuwa hakuna mpango wowote wa kujenga nyumba katika shule hiyo.

Alisema  shule  hiyo licha ya kuwa na walimu 16 inazo  nyumba tano kati ya hizo  moja  ndio  imejengwa kwa tofali za kuchoma kwa nguvu ya wananchi na nyumba  nyingine zimejengwa kwa tofali za  tope na  ziko  katika  hli mbaya ya uchakavu.

Alifafanua  kuwa  changamoto ya  nyumba za kuishi walimu  katika  shule  hiyo  imesababishwa na  Halmashauri ya Nsimbo kutotenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu  licha ya yeye  diwani kuishauri  Halmashauri  lakini  imekuwa  haitengi  fedha kwaajili ya kuboresha mazingira ya watumishi hao wa idara ya elimu.
Mwisho

No comments:

Post a Comment