Saturday 22 April 2017

TRA Sumbawanga yakamata magari ya taka

Na Gurian  Adolf
Sumbawanga
 
WAKAZI wa mji wa Sumbawanga mkoani Rukwa wako katika hatari ya kukumbwa na magonjwa ya mlipuko na pengine kupelekea vifo baada ya mamlaka ya mapato TRA kuyakamata magari yote ya kuzoa taka ya Manispaa ya Sumbawanga kwamadai kuwa yanadaiwa reseni za barabarani (Roadlicences) kiasi cha shilingi milioni7.

Magari hayo yamekamatwa tangu April 19 hali iliyisababisha mji kuwa mchafu kutikana na kushindikana kuzolewa kwa taka baada ya magari hayo kukamatwa kufuatiwa kudaiwa.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Sumbawanga Hamidu Njovu alisema kuwa ni kweli magali yao yamekamatwa na TRA na yanadaiwa kiasi hicho cha fedha lakini amejitahidi kuisihi mamlaka hiyo kuwa vumilia watalipa baada ya kupata fedha lakini wamekataa ndiyo maana wameshindwa kuzoa taka.

Alisema kuwa iwapo busara ingetumika magari hayo yaachwe yaendelee kufanya kazi ingeondoa mlundikano wa taka katika mji wa Sumbawanga lakini imekuwa ngumu na hali ilivyo ni hatari kwa afya za wananchi wa mji huo.

Njovu alisema kuwa mpaka sasa halmashauri haina namna ya kufanya mpaka hapo fedha zitakapo patikana ndiyo walipe na magari hayo yaachiwe ili yaendelee na shughuri za uzoaji taka hali ambayo inaendelea kuhatarisha usalama wa wananchi kwani haijulikani fedha hizo zitapatikana wakati gani.
mwisho

No comments:

Post a Comment