Gurian Adolf
Katavi
Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la
Vestina Peter (27) Mkazi wa Kijiji cha Ilalangulu
Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi amekutwa akiwa
ameuwawa kikatili kwa kuchomwa na Kisu tumboni hadi kupoteza
maisha.
Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari ameviambia vyombo vya habari kuwa tukio hilo la mauwaji ya kikatili
limetokea juzi majira ya saa kumi na
mbili jioni.
Amesema kabla ya tukio hilo marehemu aliaga
nyumbani kwake alikokuwa akiishi na mumewe kuwa anakwenda shambani
kwake kuvuna mahindi katika eneo
la Kazaroho.
Kidavashari ameeleza baada ya marehemu
kuelekea shambani hakuweza kurudi
nyumbani kwake kwa muda wa siku mbili hadi hapo mwili wake
ulipo onekana ukiwa shambani kwake huku ukiwa amechomwa na visu tumboni hali iliyopelekea utumbo wake
kutoka nje na akiwa na majeraha ya kuchomwa na vitu sehemu ya
kulia ya bega lake.
Amesema baada ya mwili wa marehemu huyo
kupatikani taarifa zilitolewa kwenye kituo cha Polisi cha kibaoni,
ambao walifika kwenye eneo hilo baada ya muda mfupi na chanzo cha
mauwaji ya kikatili ya mwanamke huyo bado hakifahamika.
Kamanda wa Polisi Kidavashari ameeleza kuwa
mpaka sasa jeshi la polisi linawashikilia watu
wawili kwa mahojiano zaidi, ambao ni
Charles Julio(42) Mkazi wa Ilembo na Fred Ndaina (42)
Mkazi wa Kijiji cha Ilalangulu Kata ya Kibaoni.
Aidha Amesema watuhumiwa hao wanatarajiwa
kufikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi utakapo
kuwa umekamilika ili kujibu tuhuma zinazo wakabili.
No comments:
Post a Comment