Wednesday, 3 June 2015

Ajinyonga baada ya polisi kukataa kumuweka mahabusu



Gurian   Adolf
Katavi.
 
Mtu mmoja  aliyefahamika kwa jina  la Petro  Magawe (40) Mkazi wa  Mtaa wa Ilembo  Wilaya ya Mpanda  amekutwa  akiwa  amejinyonga  kwenye mti  kwa kutumia  shati lake  alilokuwa amevaa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa  wa Katavi kamishina mwandamizi msaidizi Dhahiri Kidavashari amewaambia waandishi wa Habari kuwa tukio hilo la kujinyonga kwa mtu huyo lilitokea  katika eneo la ofisi ya misitu  katika mtaa wa Majengo A  mjini  hapo.
Kabla ya tukio hilo   marehemu huyo alifika kwenye  kituo cha Polisi  cha Wilaya ya Mpanda,  nakueleza  kuwa  anaomba  na anahitaji awekwe  mahabusu.
 Kamanda Kidavashari amesema  kauli hiyo ya marehemu  ya kuomba  awekwe mahabusu iliwashtua polisi waliokuwa zamu kwani sio jambo la kawaida kwa mtu kuomba awekwe mahabusu.
Hata Hivyo  marehemu alipatiwa msaada  wa kupewa PF 3 kwa ajiri  ya kwenda Hospitali  kupatiwa matibabu kwani alionekana  kuwa  mtu aliyechanganikiwa.
Aidha baada ya kupewa PF3 hiyo aliondoka mpaka kesho yake  mwili wa marehemu ukiwa umekutwa ukining’inia baada ya kunyongwa  kwa kutumia shati, ambapo kamanda  Kidavashari amesema chanzo cha tukio  hilo bado hakijajulikana  na jeshi la polisi  linaendelea  na uchunguzi  wa tukio hilo.

No comments:

Post a Comment