Na Gurian Adolf
Sumbawanga
KATIBU mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA)
taifa, Dr Wilbrod Slaa amewataka wakazi wa mkoa wa Rukwa kuhakikisha
wanakimwaga chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu ujao kwani ndiyo chanzo
cha wao kuwa naisha magumu ikiwemo kukosa soko la mahindi.
Akihutubia maelfu
ya wakazi wa mkoa huo ambao walifika katika viwanja vya shule ya msingi Kizwite
alisema kuwa hali mbaya inayolikabiri taifa hivi sasa ni kutokana na uongozi
mbaya wa chama cha Mapinduzi.
Alisema kuwa
chama hicho kimeshindwa kuisimamia serikali iliyopo madarakani na hivyo taifa
kukumbwa na ufisadi, wizi na ujambazi wa maliasili kiasi kwamba nchi imebaki
nyeupe na haina kitu hivi sasa.
‘’maisha ya
watanzania yanazidi kuwa magumu kwasababu ya CCM, hakuna njia nyingine kwa
watanzania zaidi ya kukibwaga chama hicho katika uchaguzi mkuu ili iundwe
serikali mpya ambayo kamwe haitawapa nafasi mafisadi ambao ndiyo wamekuwa
jinamizi wa taifa hili’’…..alisema Slaa.
Katibu mkuu
huyo alisema kuwa suluhu ya matatizo ya watanzania ni kuhakikisha
wanajiandikisha kwa wingi katika daftari la kudumu la wapigakura na mwezi wa kumi
wajitokeze kwa wingi ili kupigia kura wagombea watakaoteuliwa na UKAWA kwani
ndio wamebeba matumaini ya watanzania wote.
Aidha aliwashukuru
wakazi wa mkoa wa Rukwa kwa kukipa ushindi mkubwa chama cha CHADEMA katika uchaguzi wa
serikali za mitaa mwezi wa 12 mwaka jana
ambapo katika jumla ya mitaa 166 katika mkoa wa Rukwa CHADEMA ilipata
mitaa 102 huku CCM ikiambulia mitaa
62 tu.
No comments:
Post a Comment