Wednesday, 6 December 2017

Wananchi wasidubiri kuletewa maendeleo na serikali

Na Gurian Adolf
Sumbawanga
Naibu waziri wa ofisi ya rais tawala za mikoa,( Tamisemi )Josephat Kandege amewaambia watumishi wa umma mkoani Rukwa wawaondolee dhana wananchi kuwa kazi ya serikali ni kuwaletea maendeleo badala yake wawahimize kufanya kazi na wajibu wa  serikali ni kuwatengenezea fursa iliwaweze kufanikiwa. 

Kandege aliyasema hayo jana wakati akifanya majumuisho ya ziara yake mkoani Rukwa ambapo alizungumza na watendaji wa halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga. 

Alisema kuwa bado kunadhana kwa wananchi kuwa kazi ya serikali ni kuwaletea maendeleo matokeo yake wamekuwa wakibweteka katika kufanya kazi wakitegemea serikali itawaletea maendeleo wakati sera ya serikali ya awamu ya tano inasisitiza kila mtu afanye kazi. 

"nawaagiza waelezeni wananchi kuwa kazi ya serikali siyo kuwafanyia maendeleo mtu mmoja mmoja, bali ni kutengeneza fursa ili mwananchi atumie fursa iliyopo kujiletea maendeleo,maana wapo ambao wanataka serikali iwafanyie kila kitu, hali ambayo sio sawa kwani kazi ya serikali ni kuwahakikishia wananchi huduma za msingi Kama afya,maji,miundombinu na vinginevyo" alisema

Aidha waziri Kandege aliwaonya watumishi wa idara ya elimu mkoani humo kuacha kufanya matumizi mabaya katika fedha za capitation kwani kumekuwepo na taarifa kuwa wamekuwa wakitumia fedha hizo vibaya watambue serikali haiwezi kuvumilia kuona matumizi hayo mabaya. 

Awali alitoa akimkaribisha waziri huyokatibu tawala msaidizi wa mkoa wa Rukwa anayeshughulikia tawala za mikoa na Serikali za mitaa Albinus Mgonyani alimwambia kuwa mkoa huo unakabiliwa na deni kiasi cha  shilingi milioni 538 ambalo wakulima wanadai kupitia wakala wa chakula wa taifa NFRA mkoani humo.

Alisema wamekwisha fanya mchakato ili liweze kulipwa lakini pia alimuomba waziri huyo awasaidie kulisukuma ili lilipwe haraka kwani wakulima wanazihitaji fedha hizo ziwasaidie kununua pembejeo za kilimo  katika msimu huu ambao tayari umekwisha anza.

Mwisho

No comments:

Post a Comment