Wednesday, 6 December 2017

Gereza latakiwa kuzalisha mbegu

Na Gurian Adolf
Sumbawanga
SERIKALI mkoani Rukwa imelishauri gereza la kilimo la Mollo lililopo mkoani humo  kuanza kuzalisha mbegukwaajili ya kuwauzia wakulima ili kuwaepusha kununua mbegu bandia kutoka kwa wafanyabiashara wa pembejeo wasio waaminifu. 
Ushauri huo umetolewa jana na mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo wakati alipofanya ziara ya kutembelea gereza hilo kwalengo la kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na wafungwa.
Alisema kuwa katika mikoa ya nyanda za juu wakulima wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la kuuziwa mbegu bandia hali inayosababisha malala ya kupata hasara kwani wanazalisha chini ya kiwango. 
“Tumekuwa tunahangaika na suala la mbegu bandia katika mikoa ya Rukwa na Katavi, tunaweza kujikita katika uzalisha wa mbegu za aina tofauti ikiwemo mahindi kwa na kuwauzia wakulima  katika mikoa ya kusini na nchi tukawaepusha nakutumia mbegu bandia" alisema
Kwaupande wake mkuu wa gereza hilo ACP John Mwamgunda alimwambia mkuu huyo wa mkoa  kuwa gereza hill linalima mazao ya mahindi ya kwaajili ya chakula chawafungwa kati ya ekari 350 hadi 400 na maharage ekari 20 hadi 30 na bustani za mboga mboga kati ya ekari 2 hadi 3 na kuwa mpaka sasa wana ziada ya magunia ya mahindi ya chakula 3,263 ambayo yanatosha kwa chakula cha wafungwa mpaka msimu ujao wa mavuno.
Alisema pamoja na kuwa na kulima katika maeneo hayo vitendea kazi bado ni changamoto kwani ni vichache na vilivyopo vimechakaa, hivyo wanahitaji kuongezewa ili waweze kuzalisha  maeneo makubwa zaidi.
Katika msimu wamavuno uliopita wakikabiliwa kuvuna mshindi gunia 4,058 ambayo hutumika  kulisha magereza matatu ya mikoa ya Rukwa na Katavi.
Mwisho

No comments:

Post a Comment