Katavi
Masheikh watano kati ya sita wanaunda baraza la halmashauri ya Bawata ya mkoa wa Katavi wametangaza kujiuzuru nafasi zao kutokana na madai ya kukithiri kwa migogoro pamoja na ukiukwaji wa katiba ya Bakwata .
Masheikh hao walitangaza kujiuzuru jana mbele yawaandishi wa habari katika kikao kilichohudhuriliwa na mwenyekiti wao Sheikh shaban Bakari .
Waliotangaza kujiuzuru ni Sheikh Mashaka Nassoro Kakulukulu, Shekhe Hassani Mbaruku,Said Haruna Omary , Mohamed Shabani Sigulu na Mwenyekiti wao wa baraza la halmashauri ya Bakwata mkoa wa Katavi.
Kwa upande wake Sheikh Mashaka Nassoro Kakulukulu alisema yeye haoni sababu ya kuendelea na nafasi hiyo kwamadai kuwa mambo ya kimaendeleo yemekuwa hayaendi sawa ndani ya uongozi wa Bakwata katika mkoa huo.
Alisema kuwa hata katiba ya Bakwata imekuwa ikikiukwa na kumekuwepo na migongano wa baadhi ya maamuzi yanayotolewa na vikao halali vya kuleta maendeleo na kutenguliwa na vikao visivyo halali kwa mujibu wa katiba ya Bakwata.
Naye Shekhe Said Omary alisema sababu kubwa ya yeye kuchukua uamuzi huo wa kujiuzuru ni kutokana na mazingira ya viongozi wa Bakwata kutofuata Katiba.
Kwa upande wake sheikh Mohamed Shaban Sigulu alisema yeye ameamua kujiuuzuru kutokana na uongozi wa Bakwata kuwa na misuguano haliambayo imesababisha miradi ya maendeleo iliyopo kusimama kutokana na msuguano wa kiuongozi.
Alifafanua kuwa misuguano hiyo ya ndani ya Bakwata imesababisha hadi mwalimu wa madras I katika msikiti mkuu wa Mkoa wa Katavi kuamua kuacha kazi ya kufundisha hivi karibuni.
Mwenyekiti wa Baraza la halmashauri ya Bakwata wa Mkoa Shaban Bakari alisema yeye binafsi ameamua kujiuzuru nafasi hiyo kwaajiri ya kuwepo kwa misuguano ya uongozi ndani ya Bakwata Mkoa hali ambayo imekuwa ikisababisha baadhi ya vikao kufanyika bila kuwepo kwa wajumbe halali wa vikao hivyo.
Hivyo kutokana na sababu hizo haoni umuhimu wakuendelea kuwa mwenyekiti na badala yake ni vema watafute mtu mwingine ahukue nafasi yake.
mwisho
No comments:
Post a Comment