Sunday 1 October 2017

RC awaasa wananchi

Na Gurian Adolf
Sumbawanga
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Zelote Stephen amewatahadharisha wananchi wa Mkoa huo kuhusiana na mvua zilizoanza pamoja na upepo ulioezua baadhi ya paa za nyumba na vituo vya kutolea huduma katika maeneo mbalimbali mkoani humo.
Akizungumza na vyombo vya habari jana mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa sasa ni wakati wa wazazi kuwalinda watoto wao katika msimu huu wa mvua na kuongeza kuwa wenye nyumba hawanabudi kuimarisha majengo yao mapema ili kuweza kuepuka hasara zinazoweza kutokea. 
“Ni wakati muafaka  kila mtu kuchukua tahadhari kuangalia watoto, kukagua majengo ili kuona kama yapo imara na pale ambapo madahara yanatokea basi ajue sehemu salama ya kukimbilia ili kuokoa maisha,”
Akizungumzia suala la usafila kila jumamosi ya mwisho ya mwezi alisema kuwa sualahilo linaanzia nyumbani kwa mtu na kuwa wananchi wafanye usafi kwa faida yao wenyewe na kuendelea kuwasisitiza wakurugenzi wa Halmashauri kuendelea kusimamia usafi kuanzia ngazi ya Kijiji au mtaa ili kutekeleza agizo lake la kufanya usafi kuanzia katika ngazi hizo.
“Nimewaagiza wakurugenzi na wataalamu wake wakague usafi kwasababu suala la usafi ni faida kwa kila mtu, siyo faida ya rais wala mkuu wa mkoa pekee, kwasababu tukiingiliwa na magonjwa halitakuwa la rais peke yake,” alisema
Aidha Zelote aliwaonya watu wenye tabia ya kuchoma misitu hovyo hasa katika kipindi hiki cha kukaribia msimu wa kilimo, hivyo aliwasisitiza viongozi kuanzia ngazi ya vijiji kushirikiana kuhakikisha kuwa jambo hilo halitokei.
“Katika kipindi hiki uchomaji hovyo wa mioto unaonekana kushika kasi, ni juu ya serikali ya Kijiji ama kata kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba mioto haiwashwi  hovyo na atakayefanya hivyo achukuliwe hatua za kisheria kwani mambo haya huaribu mazingira na pia usipodhibitiwa huleta madhara,” Alisema.
Hata hivyo aliwaasa wakazi wa mkoa huo kuheshimu Sheria za nchi kwani kufanya hivyo kutasababisha kuwepo na amani na utulivu tofauti na hivyo wataiona serikali mbaya. 
Mwishou

No comments:

Post a Comment