Wednesday 12 July 2017

Kujichukulia sheria mikononi bado ni changamoto mkoani Rukwa

Na Gurian Adolf
Sumbawanga
TABIA ya baadhi ya wakazi mkoani Rukwa ya kuendelea kujichukulia hatua mkononi bado inaendelea kuota mizizi mkoani humo ambapo watu watatu  wameuawa na kisha  miili yao kuchomwa  moto wakituhumiwa kwa wizi wa ng'ombe 16.
Tukio hilo lilitokea katika   kijiji  cha Mao  kata  ya  Mbuluma   wilaya   ya Kalambo  mkoani   Rukwa ambapo watuhumiwa hao walidaiwa kuwa wameiba  ng’ombe  16    wa   Mtokambali   Nsosomo.
Akizungumza na gazeti hili diwani  wa  kata  hiyo    Saidi  Manoti, alisema  kuwa   wezi hao  walikuwa  wametokea  katika kijiji  Nchenje   wilaya  jilani  ya  Nkasi  na  kwenda kuiba ng'ombe hao katika  kijiji  jirani cha Mao.
Alisema baada ya kufanikiwa kuiba  ng'ombe hao na kuanza kuondoka nao kutoka katika kijiji hicho majira ya usiku wa manane ndipo wakazi wa kijiji hicho walipo  amshana na kwenda kuwakamata wezi  hao.
Baada ya kuwanyemelea walifanikiwa kuwazingira ndipo walipowakamata na kisha  kuwapa kipigo hali iliyowafanya washindwa  kukimbia  ndipo walipo  wachoma moto wezi  hao na kuwaua kabisa.
Aidha  alisema kuwa   watu hao hawakutambulika   majina  wala makazi yao licha ya kuwa walidhaniwa kuwa wametikea katika vijiji vya jirani na walipokwenda kufanya wizi huo wa mifugo.
Diwani huyo alisema kuwa  na kuwa kutikana na kuendelea kushamiri kwa mauaji hayo holela anaandaa utaratibu wa kuitisha mikutano ya hadhara katika kata yake  ili   kutoa  elimu   kwa wananchi  juu  ya  kuachana  na vitendo  vya  kujichukulia  sheria mkononi kwa kisingizio kuwa ni wananchi wenye  hasira Kali.
Kwa upande wake Kamanda  wa  polisi  mkoani Rukwa  Geoge  kyando, amekiri kutokea  kwa mauaji hayo ya watu sita na kuongeza kuea tayari baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mao wamekamatwa  na watafikishwa  mahakamani pindi upelelezi  utakapo kamilika.
Aidha ameendelea kuonya tabia  hiyo ya kujichukulia sheria mikononi kwa kuwaua watuhumiwa kwa kisingizio kuwa ni wananchi wenye  hasira Kali.

Mwisho

No comments:

Post a Comment