Wednesday 19 July 2017

Amuua mpenzi wake baada ya kuombwa naauri

Na Gurian Adolf
Nkasi
MSICHANA siyefahamika kwa jina wala umri wake ameuawa kwa kipigo na kisha maiti yake kufukiwa kwenye shimo huku ukiwa imewekwa  kwenye mfuko wa sandarusi.
Tukio la  mauaji ya msichana huyo lilitokea julai 18 majira ya  02.00 za asubuhi  katika kijiji cha Kate kata ya Kate wilayani Nkasi ambapo uvumi ulienea kijijini hapo kuwepo kwa mauaji na baada ya uchunguzi ndipo lilipogundulika shimo na kufukiwa porini umbali kama wa kilomita moja kutoka kijijini.
Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa George Kyando alisema kuwa baada ya kulifukua shimo hilo waliweza kuukuta mwili wa mwanamke huyo na baada ya uchunguzi wa kidaktari mwili wa marehemu ulikutwa na majeraha matatu kichwani ya kukatwa na kitu chenye ncha kali kinacho dhaniwa kuwa ni panga na chanzo cha kifo chake ni kutokwa na damu nyingi.
Akitoa ufafanuzi juu ya tukio hilo kamanda Kyando alidai kuwa marehemu alifika kijijini hapo akitokea jijini Dar es salaam ambapo inadaiwa ni mwanafunzi  na kufika kwa mwenyeji wake aliyejulikana kwa jina la Samwel selemani na kumtambulisha kwa jirani zake kuwa ni mpenzi wake.
Baada ya muda kijana huyo alitoweka nyumbani na kuelekea kusikojulikana na Mwanamke mwenyewe hakuonekana na kuwa siku chache za nyuma kulitokea ugomvi kati mwanaume na marehemu ambpo mwanamke alikua akiomba nauli ya kurudia jijini Dar es salaam kwa madai kuwa anataka arudi shule lakini Mwanaume ambaye ni mtuhumiwa alikataa kuitoa nauli hiyo akidai kuwa hataki mpenzi wake huyo aondoke.
Baada ya mvutano  wa muda mrefu ndipo mtuhumiwa alidai kumuua mapenzi wake huyo na kuufukia mwili wake kwani hakua  tayari mwanamke huyo aondoke kwani yeye alitaka  waanze kuishi pamoja wakati mwanamke huyo alikuwa hayupo tayari kwa madai kuwa ni mwanafunzi.
Marehemu hakuweza kutambulika na kuzikwa eneo la tukio,huku mtuhumiwa aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wake hajapatikana mpaka hivi sasa na jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta na iwapo atakamatwa afikishwe mbele ya sheria.
Mwisho

No comments:

Post a Comment