Thursday, 11 May 2017

Watatu wafariki dunia wakisafirisha magendo

Na Walter Mguluchuma

 Katavi.

Watu wa tatu ambao ni wakimbizi kutoka Nchi ya Burundi wanaoishi katika makazi ya wakimbizi ya Katumba mkoani Katavi wamekufa papo hapo bada ya  gari waliliokuwa wamepanda wakiwa wanasafirisha magogo kuacha njia na kisha kupinduka.

Ajari  iliyosababisha  vifo vya watu hao ilitokea Mei  8, majira ya saa 9;30 usiku  katika Kijiji cha  Kanoge, Makazi ya wakimbizi ya Katumba  Wilayani  Mpanda ambapo watu hao walikuwa wakisafirisha kwa magendo magogo ya mti wa mkurungu ambao ni kosa kisheria kukata miti hiyo.
Akitoa taarifa ya tukio hilo Kamanda wa polisi Mkoa wa  Katavi  Damas  Nyanda  alisema  kuwa  ajali hiyo ililihusisha gari lenye namba za usajiri  T 880 BNX  aina ya Mitsubish  lililokuwa likiendeshwa na  dreva  aliyejulikana kwa jina moja la Boni ambae  ndie mmiliki wa gari hilo.

Alisema gari  hilo  lilikuwa likitokea  Katumba katika  makazi ya  wakimbizi  likielekea mjini Mpanda na lilikuwa limepakia magogo hayo ya Mkurungu ambayo walikuwa wakiyasafirisha kwa magendo nyakati hizo za usiku.

Waliokufa katika ajali hiyo majina yao hayaja  julikana bado lakini ni wakimbizi wanao ihi katika makazi hayo na mili ya  marehemu hao imehifadhiwa  katika  Hositali ya  Manispaa ya  Mpanda  kwa ajiri ya kutambuliwa na ndugu zao.

Kamanda  Nyanda  alisema kuwa chanzo cha  ajali  hiyo ni kutokana na mwendo  kasi wa  dereva wa gari hilo  hali iliyosababisha  dereva wa  gari hilo kushindwa kuliumudu na kugonga  gema pembeni ya bara bara   na kisha kupinduka.

 Alisema Dreva wa  gari  hilo alikimbia mara baada ya kutokea kwa ajari hiyo na jeshi la Polisi  linaendelea na msako wa kumtafuta ili  aweze kujibu  mashitaka  yanayomkabili.

Kamanda huyo wa polisi  ametoa wito kwa madereva  kufuata  sheria za usalama barabarani na wamiliki wa magari waache tabia ya kusafirisha bidhaa ambazo ni zamagendo kwani ni hatari kwa usalama wao na vyombo vya moto wanavyo endesha.

Mwisho

No comments:

Post a Comment