Wednesday, 17 May 2017

Warembo wa Nkasi wagomea kujifunza ufundi Makenika

Na Gurian Adolf
Nkasi
 
KUTOKANA na kutojua umuhimu wa elimu kwa baadhi ya watoto wa kike wilayani Nkasi mkoani Rukwa kumesababisha baadhi ya watoto wa kike waliopewa fursa maalumu ya kulipiwa mafunzo ya ufundi wa aina mbalimbali ikiwemo ujasiliamali na makenika na shirika la Plan International, wameacha mafunzo hayo na kudai kuwa wao ni  warembo na hawafai kusomea ufundi makenika.

Hayo yamebainishwa jana na Nestory Frank mratibu wa ndoa za utotoni kutoka shirika la Plan International wilayani Nkasi Katika mafunzo ya siku mbili inayofanyika katika ukumbi wa Mtakatifu Bakita na kuwakutanisha wajumbe wa kamati ya wilaya ya kumlinda mtoto wa kike dhidi ya mimba za utotoni.

Alisema kuwa shirika hilo liliandaa program maalumu ya kuwapatia mafunzo watoto wa kike waliopata ujauzito katika umri mdogo kutoka kata tatu za Mtenga, Mkwamba na Nkandasi ili waweze kupata mafunzo hayo yatakayowasaidia kujikomboa ki uchumi baada ya kufuzu mafunzo hayo na kuanza kufanya shughuli za uzalishaji Mali kwa faida zao.

Frank alisema kuwa baadhi ya watoto hao  wakike wameamua kuacha kuhudhuria mafunzo hayo wakidai kuwa hawataki kusomea  kozi ya makenika, huku wengine wakiwa walikatisha masomo na hawajui kusoma  na kuandika lakini wanang'ang'ania kusomea fani ambazo zinahitaji elimu kubwa kitu ambacho kimekuwa ni  changamoto.

Alisema kuwa baadhi ya watoto hao wa kike  wanataka kusomea ufundi umeme ambao unahitaji elimu kubwa lakini wakishauriwa wajifunze makenika wanakataa wakidai kuwa wao ni  warembo na hawawezi kusomea Kazi kama hiyo.

Mratibu huyo wa ndoa za kutotoni alisema kuwa baadhi ya watoto hao  wa kike  wamekuwa na masharti magumu wakidai kuwa hawapo tayari kusomea baadhi ya mafunzo kama ufundi cherehani mpaka wanunuliwe cherehani na shirika la Plan International ambalo linawalipia mafunzo hayo na wakabidhiwe ziwe Mali yao ndipo wakubali kusomea mafunzo hayo.

Alisema kuwa kuna  madarasa yalikuwa na wanafunzi 25 na wameacha hadi kubakia wanafunzi wanne wengine bila kutoa sababu hali ambayo inakatisha tamaa kwani lengo la  shirika hilo  ni kuwasaidia wao waweze kujikomboa ki uchumi kwani baadhi yao walikatishwa masomo na hawana ujuzi wowote utakao wasaidia maishani ili wajikomboe kwa kujiajiri na kuajiliwa.

Frank alisema kuwa changamoto nyingine ni kuwa baadhi yao wameonekana kupata ujauzito wakiwa wanaendelea na mafunzo hayo na kulazimika kuacha kuhudhuria wakidai kuwa wanalea mimba hivyo hawapo tayari kuendelea na mafunzo.

Alisema kuwa shirika la Plan International kupitia program hiyo inamlipia kila mtoto  hadi shilingi 150,000 lakini wanaamua kuacha na kurejea mtaani na kuonekana kuwa hawahitaji kabisa mafunzo hayo na hivyo kusababisha fedha hizo kupotea kwa kuwalipia watu wasiotaka kupata ujuzi.

Bado wamekuwa wakiendelea kuwabembeleza ili warejee na kupata mafunzo hayo lakini baadhi yao wamekuwa hawataki kabisa na kuacha hali  ambayo inasababisha changamoto kubwa katika utekelezaji wa mradi huo ambao unania ya kuwasaidia wao wenyewe.

Akizungumza katika mafunzo hayo mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo Josepha  Josefu alisema kuwa miongoni mwa matatizo ni  wanawake ambao mama zao na watoto hao  wakike nao wanaridhika kuona watoto wao hao  wakiacha mafunzo na wao wanaridhika inawezekana kwa kuwa nao hawajui umuhimu wa elimu.

Alisema watoto hao  ambao wanapewa ujauzito hawaolewi na matokeao yake  wanabaki nyumbani kwao wakiwalea watoto wao kwa shida na kusababisha mzigo katika familia kwani inabidi wazazi wa mwanamke ndiyo wachukue jukumu la  kuwalea watoto wao na wajukuu na hivyo kusababisha hali ngumu katika familia kwani wazazi wao wanabeba mizigo ambayo hawakustahili.

Josefu alisema kuwa inatia aibu kuona mtoto  wa kike  aliyekatishwa ndoto zake kwa kupewa mimba katika umri mdogo lakini amepata fursa ya kupata mafunzo kwa kulipiwa na shirika la Plan International akiacha na wazazi hususani mama anaridhika  na kuona ni kawaida kitu kinachoumiza na kusikitisha.

Alisema kuwa program hiyo ni ya muda tu na itakapo malizika itawaacha katika umasikini kwani wameshindwa kuitumia vizuri na hata  watoto waliozaa watakuwa masikini kwa kuwa wazazi wao watashindwa kuwa lea  vizuri kutokana na umasikini na kama mikoa mingine wangeipata fursa hiyo Wang rich an gamma ili iwaokoe watoto hao  wakike.

Mwisho

No comments:

Post a Comment