Na Walter Mguluchuma
Katavi
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamelipongeza Shirika la umeme TANESCO katika Mkoa huo kwa kutatua matatizo ya wateja wao kwa haraka na kwa wakati pindi yanapokuwa yametokea.
Pongezi hizo zilitolewa jana na madiwani hao ambao waliongozwa na Meya wa Manispaa hiyo Willy Mbogo wakati wa ziara yao ya kutembelea mradi wa umeme wa ORIO unaofadhiliwa kwa ushirikiano baina ya Serikali ya Uholanzi na serikali ya Tanzania unaotarajiwa kukamilika mwezi huu.
Meya wa Manispaa hiyo, Mbogo alieleza kuwa huduma zinazotolewa na Tanesco mkoa wa Katavi kwa wateja wake zimeboreka tofauti na hapo awali ambapo matatizo ya wateja yalikuwa hayatatuliwi kwa wakati.
Hivi sasa shirika hilo limekuwa likitoa huduma kwa wateja muda wote hata nyakati za usiku wakati miaka ya nyuma ilikuwa ni vigumu kwa mteja kutatuliwa matatizo yao kwa haraka na kwa wakati.
Nae Haidari Sumry Diwani wa Kata ya Makanyagio alisema kuwa kumekuwa na mabadiliko makubwa ya utendaji kazi wa shirika la Tanesco Mkoani humo tofauti na hapo awali.
Kwaupande wake Diwani wa Kata ya Magamba Philipo Kalyalya alisema kuwa mradi huo walioutembelea utakapoanza kufanya kazi hivi karibuni utaleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kimaendeleo kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi.
Alisema mradi huo wa umeme wa ORIO ni wauhakika hivyo utawafanya watu wafanye shughuli zao kwa uhakika zaidi tofauti na hapo awali ambapo umeme uliopo sio wa uhakika kwani una katika katika na kuwafanya wafanyabiashara kushindwa kufanya shughuli zao vizuri hasa wenye mashine za kukoboa mpunga.
Msimamizi wa mradi huo wa ORIO Mhandisi Stephen Manda aliwaeleza Madiwani hao kuwa mradi huo wa Urio kwa hapa Nchini ni watatu kutekelezwa kwa ushirikiano na Serikali ya Uholanzii na Serikali ya Tanzania na ulianza kutekelezwa hapa nchini mwaka 2013 na tayari mradi kama huo umeisha tekelezwa katika Wilaya za Ngala na Bihalamulo Mkoani Kagera na sasa katika wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi .
Alifafanua kuwa mradi huo wa Mpanda umegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 20.5 kati ya fedha hizo mradi wa mashine mbili umegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 14 na njia za umeme zimegharimu shilingi Bilioni 6.5 na ulipangwa kukamilika mwezi wa saba mwaka huu lakini mradi huo umeweza kukamilika mapema zaidi ya matarajio kutokana na utendaji kazi mzuri na hivyo utakamilika mwezi huu wa tano.
Alisema Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamelipongeza Shirika la umeme TANESCO katika Mkoa huu kwa kutatua matatizo ya wateja wao kwa haraka na kwa wakati pindi yanapokuwa yametokea .
Pongezi hizo zilitolewa jana na Madiwani wa Manispaa ya Mpanda wliokuwa wameongozwa na Meya wa Manispaa ya Mpanda Willy Mbogo wakati wa ziara yao ya kutembelea mradi wa umeme wa ORIO uliopo katika eneo la Kampuni unaofadhiliwa kwa ushirikiano baina ya Serikali ya Uholanzi na serikali ya Tanzania unaotarajiwa kukamilika mwezi huu..
Meya wa Manispaa ya Mpanda Willy Mbogo alieleza kuwa huduma zinazotolewa na Tanesco mkoa wa Katavi kwa wateja wake zimeboreka tofauti na hapo awali ambapo matatizo ya wateja yalikuwa hayatatuliwi kwa wakati .
Hivi sasa shirika hilo limekuwa likitowa huduma kwa wateja muda wote hata nyakati za usiku wakati miaka ya hapo nyuma ilikuwa ni vigumu kwa mteja kutatuliwa matatizo yake kwa haraka na kwa wakati .
Nae Haidari Sumry Diwani wa Kata ya Makanyagio alieleza kuwa kumekuwa na mabadiliko makubwa ya utendaji wa kazi wa shirika la Tanesco Mkoani hapa tofauti na hapo awali .
Diwani wa Kata ya Magamba Philipo Kalyalya alisema kuwa mradi huo walioutembelea utakapoanza kufanya kazi hivi karibuni utaleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kimaendeleo kwa kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi .
Alisema mradi huo wa umeme wa ORIO ni wauhakika hivyo utawafanya watu wafanye shughuli zake kwa uhakika zaidi tofauti na hapo awali ambapo umeme ulikuwa sio wa uhakika kwani ulikuwa ukikatika katika na kuwafanya wafanyabiashara kushindwa kufanya shughuli zao vizuri hasa kwenye mashine za kugoboa mipunga.
Msimamizi wa mradi huo wa ORIO Mhandisi Stephen Manda aliwaeleza Madiwani hao kuwa mradi huo wa Urio kwa hapa Nchini ni watatu kutekelezwa kwa ushirikiano na Serikali ya Uholanzi na Serikali ya Tanzania na ulianzishwa mwaka 2013 na tayari mradi kama huo umeisha fanywa katika Wilaya za Ngala na Bihalamro Mkoani Kagera na sasa Mpanda Mkoani Katavi .
Alifafanua kuwa mradi huo wa Mpanda umegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 20.5 kati ya fedha hizo mradi wa mashine mbili umegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 14 na njia za umeme zimegharimu shilingi Bilioni 6.5 na ulipangwa kukamilika mwezi wa saba mwaka huu lakini mradi huo umeweza kukamilika mapema mwezi wa tano.
Alisema mashine zilizopo kwa sasa za shirika la Umeme Tanesco zimechoka kwani ni za toka mwaka 1980 ndipo zilipoanza kufanya kazi hivyo kwa sasa zimekuwa ni chakavu ndiyo maana hazina uwezo mzuri wa kufanya Kazi.
Mwisho
No comments:
Post a Comment