Saturday, 13 May 2017

Tasisi ya Brent yapania kuwakomboa wakulima wa mpunga Sumbawanga

Na Gurian  Adolf
Sumbawanga

TASISI ya Brent ambayo inajishughulisha  na kutoa elimu kwa wakulima wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa imedhamiria kuwapa elimu na hatimaye  kuleta mapinduzi makubwa kwa wakulima wa mpunga na kufanikiwa kuupiga teke umasikini.
 Shamba darasa la mpunga ilililosimamiwa na tasisi ya Brent ambayo ni mbegu aina ya SARO 5 TXD-306 lililopo katika kijiji cha Milepa wilayani Sumbawanga.

Afisa ufundi na elimu wa tasisi hiyo Faustina Kalyalya akizungumza katika shamba darasa lililopo katika kijiji cha Milepa wilayani humo ambapo walikuwa wakiadhimisha siku ya mkulima wa zao la  mpunga alisema kuwa tasisi hiyo ilianzishwa wilayani humo zaidi ya miaka mitano ililiyopita ikiwa  na lengo la  kutoa elimu kwa wakulima katika suala zima la  kilimo bora sambamba na kuongeza  thamani katika mazao yao.
Alisema kuwa wakulima wa mpunga wilayani humo bado wanalima kilimo cha kizamani bila kufuata  taratibu  za kilimo bora hali ambayo inawasababisha kutopata tija  katika kilimo wanacholima.
Baadhi ya wakulima wanaopata mafunzo kupitia tasisi ya Brent wakimsikiliza afisa kilimo wa wilaya ya Sumbawanga vijijini Habona Kyileluya

Kalyalya alisema kuwa lengo kubwa la  kutoa elimu kwa wakulima hao ni kuona wanafanikiwa ambapo ni matarajio ya tasisi hiyo kuwa kila mkulima aweze  kuvuna kwa kiwango cha gunia 40 za mpunga hali ambayo itawawezesha kuona faida katika kilimo wanacholima.
Alisema iwapo wakulima watafuata utaratibu za kilimo na kufuata maelekezo ya wakulima hakuna muujiza kuwa watabadirisha maisha yao kutokana na tija  watakazopata kutokana na kilimo cha mpunga ambacho ni ndicho kinachotegemewa katika bonde la  ziwa Rukwa.
Naye Afisa kilimo wa Wilaya ya Sumbawanga Habona Kwileluya alisema kuwa iwapo wakulima hao wakitumia mbegu ya mpunga aina  ya SARO 5 TXD-306 ambayo inaonekana kufanya vizuri katika bonde hilo watanufaika vizuri kwani asilimia kubwa ya wakazi wa bonde  hilo ni wakulima wa mahindi pamoja na mpunga.

Alisema kuwa nivizuri wakulima wakafuata maelekezo ya wataalamu wa kilimo waliopo katika maeneo yao ikiwa  ni pamoja na kulima  kwa wakati na matumizi ya pembejeo za kilimo tofauti na hivyo wasitegemee muujiza wa kupata mafanikio katika kilimo.
Naye mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Oresta Haule ambaye alikuwa  akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo alisema kuwa wakulima wanapaswa kufuata maelekezo ya wataalamu kwani kilimo ni biashara nakinalipa iwapo watafuata maelekezo.

Alisema kuwa changamoto nyingine ni wakulima kuwa na tabia  ya kuuza mazao wanayopata kidogo kidogo, kwamaana  ya kupima  kidogo katika vibakuli na kuuza kwa lengo la  kutatua mahitaji  yao mwishowe  hujikuta sehemu kubwa wakiuza kwa mtindo huo na hawanufaiki kwakua wamekuwa wakiuza kidogo kidogo.
Haule alisema kuwa pamoja na changamoto za kutokuwa na maghala ya kuhifadhia mavuno lakini wajitahidi kuyatunza na kubumilia ili wauze yanapokuwa na bei kubwa kwani nayo  ni njia ya kuongeza  thamani kwakua watauza  kwa bei kubwa wakati huo tofauti na wanapokuwa wamevuna.
Baadhi ya wakulima wa mpunga wanaopata mafunzo chini ya tasisi ya Brent wakiwa wamepumzika kivulini mara baada ya kutembelea shamba darasa lililopo kijiji cha Milepa

Awali  akizungumza katika maadhimisho hayo Mwenyekiti wa kijiji cha Milepa Chrisant Mdula aliishukuru tasisi hiyo pamoja na mbunge wa jimbo  lao la  Kwela Ignas Malocha ambae naye ni mkulima wa mpunga, daima wamekuwa wakijitoa kwa hali na Mali katika kuwasisitiza wakulima ili waweze kulima  kilimo cha kisasa ambacho kitawapa tija.
 Afisa ufundi na elimu wa tasisi hiyo Faustina Kalyalya (wakwanza kushoto) akizungumza katika shamba darasa lililopo katika kijiji cha Milepa wilayani
Alisema kuwa mwaka huu walikutana na changamoto za uhaba wa mvua hali iliyosababisha kutokuwa na maji ya kutosha lakini alisema kuwa anatarajia watafanikiwa tofauti na kulima  kwa kutumia mbegu ya Zambia ambayo wamekuwa wakitumia kwa miaka mingi  ambayo umeshindwa kabisa kufanya vizuri katika hali ya ukosefu wa maji ya kutosha kutokana na mvua kutokuwa za kutosha na katika msimu ujao wa kilimo wanafanya vizuri zaidi.
Tasisi ya Brent imeanzisha mashamba darasa katika vijiji  vya Ng'ongo, Kaoze, Ilemba, Sakalilo na Milepa pamoja na kwa vikundi vya wakulima vilivyopo katika bonde  la  ziwa Rukwa ambayo wamekuwa ni mfano kwa wakulima hao ili waweze kujifunza kilimo cha kisasa cha mpunga.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment