Sunday 30 April 2017

Kijana anusurika kifo baada ya baiskeli aliyokuwa anaendesha kugongwa na gari

Kizlen Rehan
Sumbawanga

KIJANA ambaye hakuweza kufahamika jina lake wala anapoishi amenusurika kifo  majira ya asubuhi katika maeneo ya benki ya NMB mjini Sumbawanga mkoani Rukwa,baada ya baiskeli aliyokuwa akiendesha kugongwa na gari.

Tukio hilo lilitokea ghafla Mara baada ya gari kuigonga baiskeli hiyo na kusababisha taili la  mbele kupinda  mara baada ya gari hilo kuigonga baiskeli hiyo.

Mwandishi wa habari hii alishuhudia tukio hilo ambapo anasimulia kuwa gari hilo lilipoteza uelekeo na kwenda kuigonga baiskeli hiyo.

Pamoja na kuharibika baiskeli hiyo lakini mtu ambaye jina  lake halikufahamika Mara moja aliyekuwa anaendesha baiskeli hiyo alinusurika.

Baada ya tukio hilo polisi wa usalama  barabarani walifika muda mfupi na kufanya uchunguzi wa tukio hilo.

Hata hivyo taratibu za kisheria zinaendelea kufuatia tukio hilo kwani askali hao wa usalama barabarani waliwachukua watu waliohusika na tukio hilo na kuelekea nao katika kituo cha polisi kilichopo mjini Sumbawanga.

Mwisho

No comments:

Post a Comment