Thursday 13 April 2017

Diwani apiga marufuku kugeuza misiba kuwa mikutano ya vijiji

Gurian  Adolf
Nkasi

DIWANI wa kata ya Mkwamba wilayani Nkasi, Chiluba Mwandamo amewapiga marufuku baadhi ya watendaji wa vijiji vilivyopo katika kata hiyo kuacha tabia ya kuigeuza misiba inayotokea katika vijiji vyao na kuwa mikutano ya vijiji.
Marufuku hiyo aliitoa jana katika kikao cha maendeleo ya kata hiyo WODC alipokuwa akizungumzia suala la tabia ya watendaji hao kutokuwa na utamaduni wa kuwasomea wananchi mapato na matumizi ya vijiji.
Alisema kuwa wapo baadhi ya watendaji ambao wamekuwa na tabia ya kusimama katika misiba iliyopo vijijini kwao na kuanza kutoa maagizo ya serikali kwa kisingizio kuwa wananchi hawahudhurii mikutano ya vijiji.
Diwani huyo alisema kuwa kwakuwa eneo hilo linakuwa ni lamsiba baadhi yao wanatumia mwanya huo kwakuwa wanajua watu watakua katika maombolezo na hivyo hawatakuwa na uwezo wa kuuliza maswali.
Mwandamo alisema kuwa wapo baadhi ya watendaji ambao wamekuwa wakidiriki hata kusoma mapato na matumizi ya kijiji hali ambayo si sawa kwani eneo hilo ni la maombolezo na wananchi wanakuwa na hudhuni kwa hiyo hawawezi kufuatilia taarifa za mapato na matumizi kwa ufasaha.
Alitoa wito kwa wananchi kuwafukuza katika eneo la msiba watendaji wenyetabia hiyo hiyo kwani wananpaswa wawe wanaitisha mikutano yao kwaajili ya kuzungumza na wananchi.
Mmoja wa wananchi wa kata hiyo Mariamu Kanana alimshukuru diwani huyo kwa uamuzi huo kwani alisema kuwa wananchi walikuwa wanakerwa na tabia hiyo lakini walikuwa wananshindwa kuwaambia.
Alisema kuwa watendaji hao hawanabudi kuitisha mikutano yao ya vijiji kama wananchi hawatakuwa wanahudhuria watafute njia ya kuwabana ili wahudhurie lakini si kugeuza misiba katika kata hiyo kuwa mikutano ya vijiji.
mwisho

No comments:

Post a Comment