Wednesday, 3 June 2015

Makampuni, Wachimbaji madini watakiwa kuzingatia Sheria za Mazingira

Makampuni, Wachimbaji madini watakiwa kuzingatia Sheria za Mazingira

Kampuni za uchimbaji madini, utafutaji mafuta na gesi wakiwemo wachimbaji wadogo nchini, wametakiwa kuzingatia sheria na kanuni za uhifadhi wa mazingira wakati wanapotekeleza shughuli zao, ili kuwezesha rasilimali zinazopatikana  ardhini ziweze kuwa endelevu  kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Rai hiyo imetolewa na   na Mhandisi wa Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Ephraim Mushi wakati wa Maadhimisho ya siku ya Mazingira duniani yanayoendelea kufanyika  katika viwanja vya Tangamano  Jijini, Tanga.
Mhandisi Mushi ameeleza kuwa, kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watu duniani hususan katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania    ni muhimu mahitaji yao yakaenda sambamba na rasilimali zilizopo.
“Nafahamu uelewa wa makampuni ya uchimbaji madini na utafutaji wa mafuta na gesi katika usimamizi na kutunzaji wa mazingira ni mkubwa, kwani tayari  kampuni hizo zina mpango wa usimamizi mazingira ambao umeeleza masuala yanayopaswa kuzingatiwa, lakini bado wanapaswa kuzingatia jambo hili wakati wote kutokana na umuhimu wa wake”, alieleza Mushi.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiCd-Um_usdZeGi-xPb6mLTjHTjIKZsiYKHhzwFUwrmUE0-oJPaeHCk04b7i3Vgl7XTXQ8zHVKfAKkOWN8bbQFSq3Ezlen-5kTGLnoNhDztaSSlzkaIdRxuA1Gk6iit46GOMC9_zpq_tB-0/s1600/picha+n0.+1.jpg



 Waziri wa Uchukuzi, Mheshimiwa Samwel Sitta (Mb) aliyekuwa mgeni rasmi kwa
niaba ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt . Mohamed Gharib Bilal, wakati wa
ufunguzi wa Maonesho ya Siku ya Mazingira Duniani, akimsikiliza  Mhandisi
wa Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini Ephraim Mushi wakati
alipotembelea banda la Wizara wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira
Duniani yanayoendelea  katika viwanja vya Tangamano jijini  Tanga.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjOW2eB8yf7HxR-msp1iJX8CKw4cgNrnzJyrJrlBfTzHeqHBt3nMk2fro7JVC6ohl2p0ekYI8umqR0ylfVPdhbW10oOpeGov_pp233Udp4W-ErG4KkRMpYmttW3Kkk9nh3TsRDGHqCZZ7us/s1600/picha+N0.+2.jpg

 Wanafunzi kutoka shule za msingi mbalimbali jijini Tanga, wakiangalia madini ya
ujenzi wakati walipotembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini katika
Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayoendelea  katika viwanja vya Tangamano jijiji Tanga.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh1sNH7xvGd6iTNZvXGIqAOHOhyf3A7jBDpPL6uovp4WuXzSipraO4Nw3baMs1ihkFXgRLvrjU6kRwj0XeeZLItBuK5FYnlTRj6rw9Kh65pEMHH-7ozpyfcH2YQ8mU27Iq9SSOxJ-axhYyb/s1600/picha+N0.+3.jpg

 Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano, Mhe.
Stephen Masele, akiongea jambo wakati alipotembelea banda la Wizara ya
Nishati na Madini wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani
yanayoendelea katika viwanja vya Tangamano Jijini Tanga

No comments:

Post a Comment