HUDUMA YA GOOD NEWS FOR ALL MINISTRY YAOMBA KUWEPO MJADALA WA WAZI KUJADILI TATIZO LA ULEVI NCHINI
Askofu Charles Gadi wa Huduma
ya Good News for All Ministry (kulia), akizungumza na waandishi wa
habari Dar es Salaam jana, kuhusu kuongezeka kwa joto duniani na athari
zake pamoja na tatizo la ulevi nchini ambapo kanisa hilo limeshauri
kuwepo na mjadala wa wazi kujadili jambo hilo. Kutoka kushoto ni
Mchungaji, Martin Ndaki na Katibu wa huduma hiyo, Palemo Massawe.…
Askofu Charles Gadi wa Huduma
ya Good News for All Ministry (kulia), akizungumza na waandishi wa
habari Dar es Salaam jana, kuhusu kuongezeka kwa joto duniani na athari
zake pamoja na tatizo la ulevi nchini ambapo kanisa hilo limeshauri
kuwepo na mjadala wa wazi kujadili jambo hilo. Kutoka kushoto ni
Mchungaji, Martin Ndaki na Katibu wa huduma hiyo, Palemo Massawe.
huo. Kulia ni Mchungaji Leons Kajuna.
mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Askofu Charles Gadi wa Huduma
ya Good News for All Ministry (katikati), akizungumza na waandishi wa
habari Dar es Salaam jana, kuhusu kuongezeka kwa joto duniani na athari
zake pamoja na tatizo la ulevi nchini ambapo kanisa hilo limeshauri
kuwepo na mjadala wa wazi kujadili jambo hilo. Kutoka kushoto ni
Mchungaji Martin Ndaki, Katibu wa huduma hiyo, Palemo Massawe, Mchungaji
Fabian Msimbe, Mchungaji Leons Kajuna, Mchungaji Denis Kumbiiho na
Mchungaji James Manyama.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
.........................................................................................
.........................................................................................
Taarifa kwa Umma
KUONGEZEKA KWA JOTO DUNIANI NA ATHARI ZAKE KWA NCHI ZETU NA HIVI KARIBUNI NCHI YA INDIA.
Ndugu
waandishi wa habari, nawasalimu katika jina la Yesu. Kwanza nawashukuru
kwa kufika kwenu kuja kunisikiliza. Jina langu ni Askofu Charles Gadi
wa huduma ya Good News for All Ministry.
Ndugu
waandishi wa habari napenda kuchukua nafasi hii kuzungumzia hali ya
joto la la dunia. Tunashukuru Mungu kwa nchi yetu kupata mvua nyingi
mwaka huu, ingawa baadhi yetu zilituathiri kwa njia moja ama nyingine
kutokana na mafuriko. Lakini tunapaswa kujua kuwa hali ya joto la dunia
kwa ujumla siyo nzuri hasa ukichukulia taarifa za mara kwa mara za
kupungua kwa barafu ya mlima Kilimanjaro na kuyeyuka kwa mabonge ya
barafu katika mabara ya barafu ya Actic na Antarctica. Taarifa hizo za
kisayansi zinaonyesha kuwa ongezeko hilo la joto linatokana na uharibifu
wa mazingira na kuongezeka kwa hewa ya ukaa (CO2 CARBON DAIOKSIDE).
Upungufu
wa misitu ambayo husaidia kunyonya hewa ya ukaa inayotumiwa na miti
kutengeneza chakula yaani phososynthesis na utumiaji wa madawa mbali
mbali yanayoharibu mazingira pia huchangia ongezeko hilo la Joto. Sote
ni mashuhuda wa jinsi misitu yetu inavyoendelea kuangamia kutokana na
shughuli za kibinadamu.
Ndugu
waandishi wa Habari, Hivi karibuni imeripotiwa kuwa wimbi kubwa la
upepo wa Joto (heat wave) limeikumba limeikumba nchi ya India na kuua
zaidi ya watu 2000 na bado wengine wanaendelea kupoteza maisha yao. Hiyo
si habari njema kwetu sisi tunaokaa duniani kwani jambo kama hilo
linaweza kutufika sisi wakati wowote maana hatuna kinga yoyote
inayotuzuia na ongezeko hilo la joto Duniani. Cha kusikitisha ni kuwa
waliokufa wengi ni wazee, maskini na watoto ambao hawana uwezo wa
kujikinga na wimbi hilo la joto kwani unahitaji uwe na viyoyozi (air
conditioning) au maji baridi ya kujinyunyuzia wakati wimbi hilo la joto
likipita.
Kwa
sababu hiyo tumesukumwa na Mungu kuandaa mkutano wa maombi huko India
ili Mungu atukinge na madhila hayo ya mawimbi ya hewa ya joto. Katika
safari hiyo ya India tutaambatana na wachungaji zaidi ya 10 pamoja na
waandishi wa Habari kadhaa ili kufanya maombi hayo, yatakayoambatana na
kutoa misaada kwa waathirika wa upepo joto huo. Ni muhimu kwetu kutoa
misaada kwa sababu wale walioathirika ni maskini na wahitaji wa nchi ile
na Biblia inasema kuwa unapomsaidia Maskini unamkopesha Bwana. Ina
maana Mungu anaweza kutumia sadaka hiyo kutuepusha na sisi kupata tatizo
linalofanana na hilo katika nchi yetu.
Ili
kufanikisha safari hiyo, tunawaomba wananchi wote wenye moyo kutuchangia
nauli na msaada wa kuwapelekea waathirika hao. Tunaiomba jamii ya
kiasia katika nchi yetu kusaidia katika hilo, na hata taasisi mbali
mbali za fedha na mashirika yasiyo ya kiserikali. Safari hiyo ni ya
uhamasisho na itahusisha pia kushauri au kuelimisha dhana nzima ya
utunzaji wa mazingira hasa misitu na kupunguza hewa ya ukaa inayochochea
ongezeko hilo la joto duniani.
TATIZO LA ULEVI KWA TAIFA
Ndugu
waandishi wa habari, Kuna habari kwenye vyombo mbali mbali vya habari
na mitandao ya kijamii, na hata Bungeni jambo hilo limetajwa kwamba
vijana wetu na wanandoa wengi wameathirika sana kwa ulevi wa kupindukia
utokanao na matumizi ya pombe za kienyeji zenye vilevi vikali. Eneo la
Rombo limetajwa kwa taarifa iliyotolewa na mkuu wa Wilaya hiyo na
kushuhudiwa pamoja na baadhi ya akina mama waliohojiwa na vyombo vya
habari kuwa limeathirika sana. Lakini napenda kuwaambia kuwa wilaya
hiyo ni mfano tu, hilo nitatizo la kitaifa kwani tunaona mara nyingi
katika vijiji, miji na mikoa watu walivyoathirika na ulevi, hadi
kushindwa kutimiza majukumu yao ya kulijenga taifa hilli. Pamoja na
kuwepo kwa habari ya aibu kuwa baadhi ya wanawake wanakodisha wanaume
toka nchi jirani ya Kenya, lakini kinachotakiwa kuangaliwa hapa ni hali
halisi ya kuathirika kwa wananchi wetu.
Sisi
tunatoa ushauri kuwa uwepo mjadala wa wazi juu ya tatizo hilo la ulevi
badala ya kutumia nguvu nyingi kumkemea Mkuu wa wilaya aliyejaribu
kutumia nguvu zake kukomesha unywaji huo mbaya wa pombe. Inasemekana
kuwa ndani ya wilaya hiyo kuna aina za pombe za kienyeji zaidi ya 50 na
nyingi huwekwa kweye chupa maalum kama zile za kiwandani huku zikiwa
hazina viwango vya TBS. Baadhi yake zina kilevi (Alkohol) zaidi ya
asilimia 58% jambo ambalo ni hatari kubwa kwa maini na figo za wanywaji.
Uwezekano wa kupuguza nguvu za kiume upo kwani wengi huamka asubuhi na
mapema kunywa vilevi hivyo na hivyo kushindia bila kula jambo ambalo
linawathoofisha kimaumbile.
Hivi
karibuni dada mmoja mwanasheria alitufuata na kutaka tuombe sana kwa
ajili ya tatizo la ulevi katika taifa kwa wanaume kwani amefanya
utafiti katika kazi yake na kugundua kuwa kwenye ndoa nyingi wanaume
hawana nguvu za kiume baada ya kuzoelea ulevi na wamama wengi
wanalalamika. Hii inaonyesha kwamba hili si tatizo la wilaya moja tu,
bali ni la kitaifa, na tunashauri lichukuliwe kwa uzito na kuwekewa
mjadala mpana zaidi wa kitaifa ili ufumbuzi upatikane. Tunamwomba
waziri mkuu aliundie tume ili hatua za haraka na za kimakusudi ziweze
kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na za kiroho, kwa kushirikisha wadau mbali
mbali ikiwa ni pamoja na serikali, vyombo vya sheria, vyombo vya kiroho
(viongozi wa dini) kutafuta usuluhishi.
Sisi
tunaona kuwa ni tatizo la kiroho kwani upo msemo kuwa ulevi unachangia
uzinzi, lakini kinyume chake sasa inaharibu nguvu za kiume. Ukisoma
Kumbukumbu la Torati 28:30 katika Biblia inasema, “Utaoa mke na mume
mwingine atalala naye . . . .” Andiko hilo linamaanisha mtu
aliyelaaniwa. Kama mtu akishindwa kulala na mkewe amelaaniwa.
Maana
ikiwa kwa sababu ya pombe wanawake wa Rombo wanaazima wanaume Kenya,
basi na wa Mtwara wataazima Msumbiji na wa Kagera na Kigoma wataazima
Burundi Rwanda na uganda. Sasa ikiwa ulevi huo uko nchi nzima, wale
walio mikoa ya kati wataazima wapi? Napenda muone kuwa tatizo hili
litafika pabaya kama halijachukuliwa hatua stahiki.
Kutokana
na hali hiyo tunashauri itafutwe namna ya kuwashauri wananchi na vijana
kwa ujumla nchi nzima namna ya kuepukana na ulevi huo, na pia sisi kama
viongozi wa dini kushirikiana kuwaelimisha kwa kanuni za kiroho na
kimwili, kwani bahati nzuri madhehebu mengi ya dini hukemea utumiaji wa
pombe. Pia watengenezaji wa vilevi hivyo washauriwe kutafuta miradi
mingine ya kuwaingizia kipato badala kutegemea pombe hizo zinazoumiza
vijana wetu.
Sasa
tatizo la pombe hizo za viroba na kienyeji ni tatizo kubwa kwa vijana wa
primary, secondary, waendesha bodaboda, madereva wa noa, bajaji nk hata
kupunguza kiwango cha elimu, ajali za mara kwa mara, na nguvu kazi ya
nchi kwa ujumla. Hili tatizo ni kubwa mno na linalenga kuharibu
(generation) au kizazi hiki cha vijana na kutengeneza jamii ambayo
haitafundishika au kutawalika kwa urahisi.
Tunawashukuru sana kwa kutusikiliza.
Wako Charles Gadi Mwenyekiti: GOOD NEWS FOR ALL MINISTRY.
No comments:
Post a Comment